Spika wa Seneti ya Burundi atoa Vifaa vya Michezo Kufaniksha Ligi ya Ujirani Mwema Mkoani Kigoma.
Posted on: October 6th, 2017
Uongozi wa Mkoa wa Kigoma umepokea Mipira 35 pamoja na Kombe kama kama sehemu ya maandalizi ya ligi ya Ujirani mwema itakayoanza kuchezwa Mkoani Kigoma kwa Upande wa Tanzania na Mikoa ya Cankuzo, Ruyigi, Rutana, Rumonge kwa upande wa Burundi, Burundi.
Akikabidhi mipira hiyo kwa niaba ya Mhe. Spika wa Seneti ya Burundi Bw. Yussuf Mossi ambayae ni Mshauri wa Masuala ya Michezo Nchini Burundi amesema kuwa wanajisikia furaha kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali mbali na mambo ya ulinzi na usalama, hivyo ligi ya Lake Tanganyika Cup itakuwa ya maana sana katika kuwaunganisha wananchi wan chi hizi mbili Tanzania na Burundi sit u katika Michezo bali hata katika kuchangamkia fursa mbalimbali za kimaendelo
Ligi ya Ujirani Mwema kati ya Mikoa ya Burundi inayopakana na Mkoa wa Kigoma upande wa Tanzania ‘Lake Tanganyika Cup’ itaanza kurindima katika Viwanja vya Lake Tanganyika Manispaa ya Kigoma Ujiji, na uwanja wa Umoja ulioko Halmashauri ya Mji wa Kasulu kuanzia tarehe 08 hadi 13 Oktoba 2017.
mchezo wa soka ni utekelezaji wa maazimio ya vikao vya Ujirani Mwema ambapo kikao cha ujirani mwema kati ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Kigoma upande wa Tanzania kikihusisha Mikoa ya Cankuzo, Ruyigi, Rutana, Rumonge na Makamba kwa upande wa Burundi kilichofanyika tarehe 29 Julai, 2017 Mkoani Makamba nchini Burundi, kilikubaliana kuanzisha ligi ya ujirani mwema kwenye mchezo wa soka kati ya Mikoa hiyo na Wilaya za Mkoa wa Kigoma pamoja na Wilaya ya Ngara kwa Mkoa wa Kagera.
Akizugumza katika hafla ya kupokea mipira 35 iliyotolewa na Rais wa Chama cha Mpira Nchini Burundi ambaye pia ni Spika wa seneti ya Burundi Bw. Reverien Ndikuriyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma amewashukuru wajumbe kutoka Burundi na kumshukuru Mhe. Spika wa seneti ya Burundi kwa kutoa mipira 35 na Kombe kwaajili ya kufanikisha Ligi ya Lake Tanganyika Cup.
“Naomba mfikishe shukrani nyingi kwa Mhe. Spika wa seneti ya Burundi Bw. Everien kwa mchango wake mkubwa katika kufanikisha ligi hii ya ujirani mwema, hii inaonesha namna gani anvyopenda michezo, ushirikiano na urafiki kwa kuimarisha michezo” alsema Bw. Pallangyo
Aidha ameongeza kuwa Ligi hii mbali na kuwa sehemu ya kuimarisha afya ni moja ya hatua ya kuimarisha mahusiano zaidi ya Mikoa jirani ya Burundi na Tanzania na wananchi wake, kwani michezo hujenga urafiki, udugu, kufahamiana na huleta furaha na maelewano.
Naye Afisa Utamaduni wa Mkoa wa Kigoma ambaye pia ni Kaimu Afisa Michezo Bw. Revocatus Lutera ameeleza kuwa Ligi hiyo imepangwa katika makundi mawili A na B, kwa timu zitakazoshiriki, kundi A ambalo linajumuisha Timu za Wilaya Kigoma, Uvinza, Buhigwe, Mashujaa FC na Mwamgongo FC litatumia uwanja wa Lake Tanganyika ulioko Manispaa ya Kigoma Ujiji. Kundi hilo lina. Kundi la B lenye timu za Wilaya ya Kasulu, Kibondo, Kakonko na Ngara litatumia uwanja wa Umoja ulioko Halmashauri ya Mji Kasulu.
Timu zitakazoshinda kutoka kila kundi zitakutana uwanja wa Lake Tanganyika kuendelea na hatua ya Robo fainali na hatimaye fainali siku ya tarehe 28 Oktoba, 2017.