Wazazi wametakiwa kuwajibika ipasavyo katika kuwalinda na kuwakinga watoto dhidi ya changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo unyanyasaji, utumikishwaaji, ajira za watoto, lishe duni, kutowapa elimu, na mambo mengine yanayoashiria kuhatarisha maisha na ndoto za watoto.
Haya yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe Brigedia Jenerali emannuel Maganga wakati wa Maadhimisho ya sherehe za kumbukumbu ya Mtoto wa Afrika Mwaka 2017, zilizofanyika katika shule ya Msingi Karuta Mkoani Kigoma.
Siku ya mtoto wa Afrika ni siku muhimu katika kutafakari mambo mbalimbali yanayomuhusu mtoto, ikiwemo malazi bora, haki za mtoto. “Katika ulimwengu wa leo wenye Changamoto, watoto wetu wanakumbana na matizo mabambali ya kimaisha na Kijamii; ni vizuri kama wazazi tukafahamu changamoto hizo na kuzitatua ili watoto wetu waisi maisha ya ndoto zao” alisema Maganga.
Aidha Mkuu wa Mkoa amelipongeza Shirika la Compassion Mission linaloshirikiana na Makanisa ya Kipentekoste Mkoani Kigoma kwa kujishugulisha kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu na wanaotoka famiia maskini, amesema ni vizuri jamii yote ikatambua kuwa kila mzazi analojukumu la kumwandalia mazingira mazuri mtoto kimaisha, kutimiza haki za mtoto pamoja na kumlinda dhidi ya manyanyaso ya aina yoyote ya mtoto kukosa haki zake.
Aliongeza kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa unaofanywa na Taasisi za kidini katika kuleta maendeleo ya watanzania kweye sekta mbalimbali , jitihada hizi zinaonekana wazi katika utoaji wa huduma kwenye jamii, hii ni ishara kuwa Taasisi za kidini zipo bega kwa bega katika kuiunga mkoano Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha mazingira bora kwa watoto na jamii.
Serikali itaendelea kuunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na wadau katika kusaidia jamii kulinda haki za watoto na kuwasaidia watoto waishio katika mazingira magumu.
Kauli mbiu ya madhimisho ya Siku ya Mtoto wa Afrika mwaka 2017 ni Maendeleo endelevu 2030: imarisha ulinzi na fursa sawa kwa watoto.