Vifaa tiba vyenye tahamani ya Shilingi Milioni 477 vimekabidhiwa kwa Uongozi wa Mkoa wa Kigoma kutoka Shirika la World Vision Tanzania pamoja na Shirika la Misaada la Serikali ya Canada-Global Affairs vilivyonunuliwa kwa ajili ya kuboresha upatikanaji na utumiaji wa huduma bora za afya kwa mama wajawazito na watoto wachanga.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (Mst.) Emmanuel Maganga akipokea vifaa hivyo, amelipongeza Shirika hilo kwa kuungana na Serikali katika kupambana na adui wa maendeleo katika Sekta ya Afya na kutoa wito kwa mashirika mengine kufuata nyayo za World Vision, mara nyingi tumekuwa tukiitwa kwenye hafla za kuzindua miradi mbalimbali inayoanzishwa lakini ninyi mmeonesha vitendo kuwa mradi wenu unagusa maisha ya wananchi wa Kigoma, nawapongeza sana na kuwashukuru.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Mgawanyo umeratibiwa na ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Paul Chaote ameeleza kuwa Vifaa tiba hivyo vitagawanywa kwa Halmashauri 6 za Kigoma DC, Kasulu DC, Uvinza, Buhigwe, Kibondo na Kakonko ambazo ndizo zimeoneka zinaupungufu na uhitaji Mkubwa wa vifaa hivyo katika vituo vya afya.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa