SHIRIKA LA THAMINI UHAI LAKABIDHI MSAADA WA PIKIPIKI ZA MIGUU MITATU KIGOMA
Posted on: September 11th, 2017
Shirika la thamini Uhai limekabidhi Msaada wa pikipiki 3 za miguu mitatu zitakazotumika kusaidia rufaa za kinamama wajawazito walio katika dharuara za uzazi maeneo ya vijijini.
Msaada wa Pikipiki hizo zenye thamani ya Shiligi Milioni 24 umetolewa Wilayani Uvinza umelenga kuvisaidia vijiji vilivyopo kata ya Nguruka.
Akizugumza katika hafla ya kukabidhi pikipiki hizo Mkurugezi Mtedaji wa Shirika la Thamini Uhai Dkt. Nguke Mwakatudu, alisema pamoja na msaada huo shirika limekuwa likishirikiana na Serikali na Wadau mbalimbali katika sekta ya Afya ambapo hadi sasa limewajegea uwezo watumisi wa Sekta ya Afya 100 na kuboresha upatikaaji wa huduma timilifu za dharula za uzazi katika vituo 12 vya afya na hospitali 3 katika Mkoa wa Kigoma pamoja na huduma za kawaida za dharula za uzazi katika Zahanati 18.
Aliongeza kuwa shirika pia limejega vumba vya upasuaji na kutoa vifaa tiba stahiki, wodi za wazazi, kuboresa mifumo ya maji na umeme.
Akizugumza mara baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakazi na wananchi wa Vijiji hivyo kutumia msaada huo ipasavo “ wafadhili watafurahi zidi tukitumia misaada hii kama iavyokususdiwa, itashagaza kuona kinamama bado wanajifungulia nyumbani wakati usafiri umeshatolewa kwa huduma hiyo, nawaomba tutumie pikipiki hizi kwa kazi iliyokusudiwa na wafadili” alisisitiza Magaga.
Magaga pia ameutaka Uongozi wa Wilaya kuhakikisa pikipiki hizo hazitumiki kinyume na kazi yake iliokusudiwa “ Mkuu wa Wilaya hakikisha pikipiki hizi hazitumiki kinyume, mtu yeyote atakayebainika kutumia kwa mambo mengine akamatwe mara moja.