Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brig. Jen. (Mst.) Emmanuel Maganga hatimaye amewahakikishia kuanza kulipwa fedha za kifuta jasho wachi walioathirika wakati wa upanuzi wa Kambi ya Wakimbiz Nduta Wilayani Kibondo.
Akizungumza kwenye mkutano na wananchi hao Mkuu wa Mkoa amesema Shirika la kuhudumia wakimbizi duniani 'UNHCR' kwa kishirikiana limefikia makubaliano ya kulipa kiasi cha Shilingi milioni 600 milioni ambazo zitatumika kufuta jasho kwa wananchi ambao walikuwa na mazao mbalimbali katika eneo hilo.
Wananchi hao wapatao 427 wanatarajiwa kulipwa fedha za kifuta jasho baada ya kupisha upanuzi wa Kambi ya Wakimbizi ya Nduta na hivyo kuathiri mazao waliyokuwa wamelima kwa kipindi hicho
Fedha hizo ambazo zitalipwa kwa awamu mbili tayari Shilingi milioni 300 zimeshaandaliwa UNHCR zitaanza kulipwa kwa wahusika mara tu watakapomaliza taratibu za kufungua akaunti na kuhakiki taarifa zao kabla ya ya Mwezi oktaba mwaka huu.
Kwa upande wao wananchi wamefurahi hatua iliyofikiwa ya kulipwa kifuta jasho kwani jambo hilo limechukua muda mrefu tangu wakimbizi walipoingia kwa wingi mwaka 2015 baada ya machafuko ya kisiasa nchini Burundi.
Kambi ya wakimbizi ya Nduta iliyopo Wilayani Kibondo ndiyo kambi yenye wakimbizi wengi Mkoani Kigoma, ambapo machafuko ya kisiasa nchini Burundi mwaka 2015 yalipelekea kambi hiyo kupanuliwa ili kuweza kutosheleza mahitaji ya wakimbizi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa