Katika kukabiliana na uharibifu wa Mazingira Mkoani Kigoma Mawaziri kutoka katika Wizara sita za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa, Ofisi ya Makamu wa rais Mazingira, Maliasili na Utaliii, Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, wakiwemo Makatibu Wakuu wa Wizara hizo walipiga kambi Mkoani Kigoma kwa lengo la kupata suluhu ya changamoto hiyo na kutoa tamko la Serikali.
Akisoma tamko hilo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Selemani Jafo (Mb) amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kukabiliana na changamoto za Uvamizi wa hifadhi za misitu na maeneo katika Mkoa wa kigoma na kusababisha migogoro kati ya maeneo yaliyohifadhiwa na wadau mbalimbali wakiwemo wananchi wanaoishi ndani au wanaopakana na hifadhi hizo.
Kutokana na tathmikni iliyofanyika hivi karibuni katika Mkoa wa Kigoma, imeonesha kuwa hifadhi za misitu na mapori ya akiba yamevamiwa kwa shughuli za kilimo, ufugaji, ukataji miti na ujenzi wa makazi ambao umesababisha athasri kubwa.
Athari hizo zimetajwa ni pamoja na kupote kwa wanyama na uoto wa asili, uharibifu wa vyanzo vya maji ikiwemo mito mikubwa kama Malagarasi, ongezekelo la mmomonyoko wa udongo ambalo linawezakutishia kupungua kina cha ziwa Tanzangyika na kupungua kwa bioanuai.
Kufuatia tamko hilo Waziri Jafo ametaja hatua zitakazochukuliwa na Serikali ili kunusuru hali ya hifadhi na mapori ni pamoja na kufanyika kwa operesheni ya kuwaondoa wavamizi wote wanaofanya shuguli mbambali bila utaratibu katika misitu na mapori Mkoani Kigoma.
Aidha kutokana na Serikali kumega zaidi ya hekta elfu kumi kutoka hifadhi ya Misitu wa Makere Kusini na kuzitoa kwa vijiji vya Mvinza na Kagerankanda, Serikali itaandaa mpango mahususi wa matumizi bora ya ardhi ilinkuwezesha zoezi la ugawaji wa maeneo hayo kufanyika vizuri. Aidha, kwa upande wa wafugaji Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetenga hekta elfu ishirini kutoka katika maeneo mbalimbali Mkoani Kigoma kwaajili ya ufugaji wenye tija
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255738192977
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa