KATIBU TAWALA MKOA WA KIGOMA HASSAN RUGWA AKIZUNGUMZA NA WADAU WANAOTEKELEZA MRADI WA SHULE BORA MKOANI KIGOMA( HAWAPO PICHANI) WALIPOTEMBELEA MKOANI HAPA KWA LENGO LA KUANGALIA MAENDELEO YA UTEKELEZAJI WA MRADI HUO KATIKA MAENEO YA UJIFUNZAJI NA UFUNDISHAJI, USHIRIKIANO WA WALIMU NA WAZAZI(UWAWA) PAMOJA NA MAFUNZO ENDELEVU YA WALIMU KAZINI (MEWAKA)
Na. GLADNESS KUSAGA-KIGOMA.
Serikali mkoani Kigoma imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa Elimu ikiwemo Mradi wa Shule Bora ili kuboresha na kuimarisha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji ili kuendelea kuinua ubora wa Elimu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa alipokutana na kuzungumza na wadau wa Elimu wanaotekeleza mradi wa Shule Bora mkoani Kigoma na kusisitiza kuwa lengo la serikali ni kuona ubora wa Taaluma unaendelea kuimarika kutokana na maboresho ya Mazingira ya utoaji na upataji wa Elimu.
Amesema Serikali kupitia watendaji wa Sekta hiyo mkoani hapa wataendelea kushirikiana na wadau ili kupunguza changamoto zinazochangia kuzorotesha na kutofikiwa kwa malengo ya serikali katika utekelezaji wa mipango ya kitaaluma sambamba na mdondoko wa wanafunzi.
Kiongozi wa Programu ya Shule Bora Taifa, Virginie Briand ameeleza kuwa mradi wa shule bora una lengo la kumuwezesha mwalimu kutekeleza majukumu yake kwa usahihi kupitia mafunzo wanayopatiwa sambamba na kusaidia zoezi la upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wakiwa shuleni ili kufanikisha zoezi la ujifunzaji na ufundishaji.
Amesema kwamba vyumb vinavyotumika kutolea Elimu lazima viakisi picha halisi ya Mazingira ya ujifunzaji hali itakayopelekea kupunguza utoro na kuwafanya wanafunzi kuhudhuria vipindi madarasani bila kutoroka na kuhakikisha walimu na wazazi wanasimamia zoezi la upatikanaji wa chakula kwa watoto ili kuhakikisha watoto wanapata utulivu muda wa kujifunza.
Akizungumza na watendaji na wadau wa Sekta ya Elimu katika Kata ya Kidahwe, wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Msaidizi wa Elimu Msingi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Susana Nussu amewataka wazazi kushirikiana na walimu kwa kufuatilia mahudhurio ya watoto na kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali kupitia miradi ya Elimu ya Kujitegemea (EK) iliyopo katika mazingira ya shule.
Bi. Susana amewakumbusha walimu mkoani Kigoma kujenga utamaduni wa kufanya Tathmini za mara kwa mara wakati wa ufundishaji na baada ya ufanyikaji wa mitihani ili kutambua maeneo yenye changamoto na mafanikio kisha kuchukua hatua ikiwemo kurudia mada, kutoa mazoezi ya kutosha kwa lengo la kuimarisha uelewa wa wanafunzi wao.
Aidha, Sasana amesema kuwa mbinu jumuishi za ufundushaji zitasaidia kukabiliana na changamoto ya utoshelevu wa walimu kwa ajili ya kufundisha baadhi ya masomo na kuondoa pengo lililopo la kufikisha huduma za kitaaluma kwa wanafunzi.
Upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Matendo Victor Gideon amesemaa Mradi wa Shule Bora kupitia programu ya Ushirikiano wa Walimu na wazazi shuleni (UWAWA) imeleta mafanikio makubwa ikiwemo kuhamasisha wanafunzi kuhudhuria shule na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa shule hiyo.
Amesema kupitia Programu ya Mafunzo Endelevu ya Walimu Kazini(MMEWAKA) pamoja na UWAWA, Shule ya Msingi Kidahwe ilipata jumla ya Shilingi 110,600,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne (4) vya Madarasa na matundu matatu (3) ya vyoo, pamoja na walimu kupatiwa mafunzo kazi ili kuwajengea uwezo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa