Baadhi ya wakazi waliojitokeza kushirikI Kilele cha Maadhimisho ya Nanenane katika Viwanja vya Ipuli katika Manispaa ya Tabora wakifuatilia Hotuba ya Mgeni Rasmi (hayupo pichani).
Maonesho ya Nanenane yamefikia Tamati leo Agosti 8, 2025 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Balozi Simon Sirro alikuwa Mgeni rasmi, ambapo katika Hotuba yake amewataka wanaoratibu maonesho hayo kuandaa mpango mahususi wa matumizi ya uwanja wa Ipuli unaotumika kikanda ili uweze kuwa kitovu cha kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo, mifugo na Uvuvi.
Amesema Taasisi zote zinazoshiriki zinapaswa kujenga majengo yenye kukidhi hadhi ya kitaifa na kimataifa na yawe ya kudumu.
MKUU WA MKOA WA KIGOMA BALOZI SIMON SIRRO AKIZUNGUMZA WAKATI AKIHITIMISHA RASMI MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MAGHARIBI AGOSTI 8, 2025.
Akizungumzia hitaji la Kanda kuongeza Thamani ya mazao kwa ajili ya Soko la ndani na nje, Sirro amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi mbalimbali za Serikali ziweke mikakati ya kuwajengea uwezo wakulima.
Akizungumzia umuhimu wa Maonesho hayo Sirro amewataka wataalam wa Kilimo, Mifugo, uvuvi, Viwanda na Biashara kuwasaidia wazalishaji na wafanyabiashara kupata masoko ndani na nje ya nchi.
Aidha Mkuu wa Mkoa amewakumbusha Watendaji na Wataalamu jukumu la kuwatembelea wakulima na kujua mahitaji, na changamoto zinazowakabiki katika uzalishaji.
Katika hatua nyingine Sirro ameyaomba Makampuni ya Mawasiliano na Taasisi za fedha kuona namna bora ya kuratibu maonesho hayo na kutumia fursa hiyo kujitangaza kutokana na ufadhili watakaokua wameufanya.Mao
MKUU WA WILAYA YA KASULU KAN. ISACK MWAKISU AKIFUATILIA HOTUBA YA MGENI RASMI WAKATI WA KILELE CHA MAONESHO YA NANENANE KANDA YA MAGHARIBI.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa