Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ametoa Tahadhari kwa wananchi wa Mkoa wa Kigoma kuchukua hatua zote zinazoelekezwa na wataalam wa AFYA kujikinga na Ugonjwa wa UVIKO 19.
Andengenye ametoa Tahadhari hiyo Wakati wa kuwasilisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2020 kwa kipindi cha mwaka Mmoja.
Amesema hali ya ugonjwa wa UVIKO 19 kwa Mkoa wa Kigoma ni nzuri ila kwasababu hali ya nchi jirani sio nzuri, ametoa wito kuhakikisha wananchi wanachukua tahadhari ya kuambukizwa kwa kufanya Kunawa Mikono kwa maji tiririka na sabuni, Kuepuka misongamono isiyo ya lazima, Kuvaa barakoa ukiwa kwenye maeneo ya msongamano na kwenye ofisi/ maeneo ambapo mzunguko wa hewa ni mdogo, Kukaa umbali wa mita tatu, Kufanya mazoezi na Kula lishe bora
Maelekezo mengine aliyoyatoa Mkuu wa Mkoa huyo ni Pamoja na Maeneo yote ya kutolea huduma za kiserikali, taasisi mbalimbali (Kama vile benki nk) watu wavae barakoa, Elimu iendelee kutolewa maeneo yote kama vile sehemu za ibada, sokoni, mashuleni na maeneo ya stendi.Wamiliki wa vyombo vya usafiri, wahakikishe wasafiri wanavaa barakoa na kunawa mikmono au kutakasa na vipukusi mara kwa mara
Aisha amewataka kila mfanyaboiashara ahakikishe kuna sehemu ya kunawia mikono kwenye eneo lake la Biashara
Viongozi wote mlioko hapa simamieni kuhakikisha kuwa tahadhari zinachukuliwa, maana kuna sehemu kuna vifaa vya kunawia mikono matumizi yake ni hafifu(hakuna maji, hakuna sabuni)
Na amewaomba Pamoja na kuchukua hatua hizo pia kila mmoja kuzidi kumuomba Mungu kila mtu kwa imani yake ili Mungu atuepushe na hili janga la UVIKO 19
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa