Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Adengenye amesema Jeshi la Polisi Mkoani humo halijawahi kumuagiza Afisa yeyote wa idara ya Uhamiaji wala Jeshi la Polisi kufanya kazi kinyume na miongozo na utaratibu na kwamba hakua maagizo ya Serikali kwa Jeshi la Polisi la kuwanyanyasa Wananchi kwa kigezo cha uraia.
Akiongea wakati wa kujibu hoja iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kigoma mjini Mhe.Kirumbe Ng’enda wakati wa Kikao cha Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi cha kuwasilisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2015 – 2020 kuhusu malalamiko ya Wananchi wa Mkoa wa Kigoma dhidi ya Maafisa wa Uhamiaji kuwanyanyasa Wananchi katika masuala ya uraia Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias andengenye alisema wataendelea kufanyia kazi malalamiko yaliyotolewa.
amesema malalamiko yanayotolewa dhidi ya maafisa wa idara ya Uhamiaji si utendaji wa Watumishi wa idara yote, isipokuwa kuna baadhi ya maafisa wa idara hiyo huenda wanatenda kinyume na sheria za uhamiaji na kuwataka kuacha mara moja kufanya hivyo lakini ifahamike kwamba Jeshi la polisi linafanya kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu na kwamba si nia ya jeshi hilo kumuonea mwananchi, na kama kunamaafisa wa Idara ya Uhamiaji wanatenda kinyume na miongozo ya kazi zao Serikali itachukua hatua dhidi yao aliongeza.
Andengenye amesisitiza Maafisa wa Idara ya Uhamiaji wanaojihusisha na vitendo vilivyo kinyume na utendaji wa Sheria za Uhamiaji kuacha maramoja, sambamba na hilo amewaomba viongozi mbalimbali Mkoani Kigoma pamoja na Wananchi kutoa taarifa mara moja wanapoona hali ya kutotendewa haki na idara ya uhamiaji.
Idara ya Uhamiaji Mkoani Kigoma imelalamikiwa kwa kutesa na kunyanyasa Wananchi kwa kisingizio cha uaraia ambapo imedaiwa kuwa baadhi ya maafisa wamekuwa wakikamata watu na kuwaambia kuwa siyo raia wa Tanzania na kuwanyanyasa na kuwaweka mahabusu jambo ambalo linatweza ubinadamu.
Aidha sababu nyingine imedaiwa ni kuwakamata watu kwa kigezo cha kuangalia majina yanayofanana na majina ya nchi jirani hali ambayo Mbunge wa Kigoma Mjini ameilalamikia Idara ya Uhamiaji kuwa si sawa na imekuwa njia ya maafisa hao wasio waaminifu kujipatia rushwa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa