• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

RC ANDENGENYE AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA WAFANYABIASHARA NDOGONDOGO

Posted on: December 12th, 2024

Wafanyabiashara  ndogondogo mkoani Kigoma wametakiwa kutumia vitambulisho vya kisasa vya wafanyabiashara kwa lengo la kujenga Mazingira rafiki ya kibiashara na kujinufaisha kiuchumi.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ametoa wito huo alipozungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya wafanyabiashara kwa mkoa wa Kigoma ambapo jumla ya vitambulisho 1453 vimegawiwa kwa awamu ya kwanza katika Halmashauri nane za mkoa wa Kigoma.

Amesema vitambulisho hivyo vimeunganishwa na mfumo wa NIDA na kimetengenezwa kwa Teknolojia inayomwezesha mtumiaji kufanya miamala ya kifedha na kukitumia kama dhamana.

Kupitia hotuba yake, Andengenye ametoa wito kwa Uongozi wa Halmashauri za Mkoa kuendelea na zoezi la utambuzi na usajili wa wafanyabiashara kwa ajili ya kupata vitambulisho hivyo sambamba na kuhamasisha wafanyabiashara kuendelea kujisaji kupata vitambulisho hivyo kwa wakati.

Andengenye ameishukuru serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kuweka mifumo rafiki ya kibiashara kwa wafanyabiashara wadogo, wakati na wale wenye mitaji mikubwa mkoani Kigoma sambamba kuendelea kuimarisha miundombinu wezeshi ili kulifanya kundi hilo kufikia malengo waliyojiwekea na kuimarisha uchumi wa nchi.

Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bi. Mwajuma Ali amesema mpaka kufikia Desemba 2024 mkoa umefanikiwa kusajili wafanyabiashara ndogondogo 2578 ambapo lengo ni kusajili wafanyabiashara  zaidi ya 5500 ifikapo Juni,2025.

Mwajuma ametoa mchanganuo wa ugawaji wa vitambulisho hivyo ambapo Halmashauri ya wilaya ya Buhigwe imepata vitambulisho 13, Kasulu 355, Kakonko 302, Kibondo 154, Kigoma 94, Uvinza 202, Manispaa ya Kigoma Ujiji 250 pamoja na Hamlashauri yaMji wa Kasulu vitambulisho 83.

Aidha, amewasisitiza wafanyabiashara ndogondogo mkoani Kigoma kuendelea kujisajili ili waweze kuingia kwenye mfumo huo wa kisasa ambapo mpaka kufikia Desemba 12, 2024 jumla ya wafanyabiashara 2578 wamekwisha sajiliwa sambamba na kulipia Ada ya usajili.

Upande wake mnufaika wa vitambulisho hivyo na mfanyabiashara ndogondogo  Manispaa ya Kigoma Ujiji John Mbuwa amesema vitambulisho hivyo vimekuwa ni sehemu ya kurasimisha biashara zao.

Amesema utaratibu huo utawapa uhuru wajasiriamali wadogo hususani waliopo katika sekta ya Biashara.

Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • RC ANDENGENYE AKABIDHI VITENGO VITENGO VYA LISHE MKOA NA WILAYA UVINZA

    May 09, 2025
  • DCP NARCIS MISSAMA AFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA

    May 07, 2025
  • JAJI ASINA AKAGUA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI-KIGOMA

    May 03, 2025
  • VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISIGEUKE MAHAKAMA ZA KUWAHUKUMU WATUMISHI-RC ANDENGENYE

    May 01, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa