MKUU WA MKOA WA KIGOMA CGF(Rtd) THOBIAS ANDENGENYE AKIWASILI KATIKA UWANJA WA ZAHANATI YA RUSIMBI NA KUPOKELEWA NA MKUU KATIBU TAWALA MKOA MHE. HASSAN RUGWA KABLA YA KUZINDUA RASMI ZOEZI LA UGAWAJI WA VYANDARUA KWA MKOA WA KIGOMA.
MKUU WA MKOA WA KIGOMA(KUSHOTO) AKITETA JAMBO NA KATIBU TAWALA MKOA MHE. HASSAN RUGWA WAKIWA KWENYE HAFLA FUPI YA KUZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI WA VYANDARUA KIMKOA LILILOFANYIKA KATIKA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
MKUU WA MKOA WA KIGOMA MHE. THOBIAS ANDENGENYE AKIKATA UTEPE KUASHIRIA UZINDUZI RASMI WA ZOEZI LA UGAWAJI WA VYANDARUA KIMKOA.
Jumla ya kaya 503,762 zinatarajiwa kunufaika na mpango wa ugawaji wa vyandarua 1,775,359 vinavyotolewa na Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ikiwa ni utekelezaji Mpango wa Taifa wa kudhibiti Maralia (NMCP) ambapo Mkoa wa Kigoma ni miongoni mwa mikoa yenye kiwango kikubwa cha maambukizi.
Akizindua rasmi zoezi la ugawaji wa vyandarua hivyo kupitia hafla fupi iliyofanyika katika Zahanati
ya Mtaa wa Rusindi Manispaa ya Kigoma Ujiji, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema kwa mujibu wa taarifa zinazotolewa kupitia mfumo wa kutolea taarifa za wagonjwa (TDHS), kwa mwaka 2024 jumla ya wagonjwa 309,080 walibainika na maambukizi ya ugonjwa huo kimkoa, ambapo idadi ya vifo ilikuwa watu 264 vikihusisha watoto 177 na watu wazima 87.
MKUU WA MKOA WA KIGOMA MHE. THOBIAS ANDENGENYE MARA BAADA YA KUKATA UTEPE KUASHIRIA KUZINDULIWA RASMI KWA ZOEZI LA UGAWAJI WA VYANDARUA MKOANI KIGOMA
Amesema vyandarua hivyo vinatolewa bure na serikali hivyo wasimamizi wanapaswa kusimamia vizuri zoezi la ugawaji ili viwafikie walengwa huku akitoa wito kwa wanufaika kufanya matumizi sahihi ili viweze kuleta tija katika kukabiliana na maambukizi ya ugonjwa wa maralia mkoani Kigoma na nchini kwa ujumla.
Aidha amewataka walengwa katika halmashauri zote nane za mkoa ambao watanufaika na mgao huo kuvitumia vyandarua hivyo kwa usahihi na kuachana na dhana potofu kuwa matumizi yake yanaweza kuchangia kupunguza nguvu za kiume au kusababisha changamoto za uzazi kwa wanawake.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema zoezi la ugawaji wa vyandarua hivyo litazigusa kaya zote mkoani Kigoma.
Amesema wakazi wa Kigoma wameendelea kuwa mashuhuda kwa ā°kujionea namna serikali ya awamu ya sita inavyoendelea kuwagusa wananchi kupitia uboreshaji mkubwa katika utoaji wa huduma za Afya nchini.
Victor Sungusia, Afisa Ugavi MSD amewataka wananchi kutumia vyandarua hivyo kwa lengo la kujikinga na maralia ili kutumia muda wao katika kufanya kazi za maendeleo badala ya kushinda wakisguhulikia changamoto za kiafya zitokanazo na maradhi hayo.
Amesema vyandarua hivyo vitatoelewa kwa kila kaya ambao kupitia mpango huo maeneo yote ya mkoa yatafikiwa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa