Iwapo Jamii itazingatia ulishaji unaozingatia lishe bora kwa watoto, itajenga msingi mzuri kwa makuzi ya watoto hao na kusababisha uwepo cha kizazi chenye weledi, uadilifu na Afya bora.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye alipozungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa ajili ya uratibu wa Shughuli za Lishe na kusisitiza kuwa jamii bora hujengwa na Msingi wa Lishe bora ili kupata kizazi chenye utimamu katika usimamizi na utekelezaji wa majukumu kwa manufaa binafsi na taifa kwa ujumla.
Amesema utekelezaji wa Afua za lishe ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) 2020 hadi 2025, kwa kuwa matokeo bora ya lishe yanahitaji ufuatiliaji wa karibu na usimamizi madhubuti ili kuhakikisha malengo yaliyowekwa na serikali yanafikiwa.
Awali Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema uwepo wa nyenzo hizo utachangia kufikia ufanisi katika malengo ya serikali kwenye utekekezaji wa afua za lishe.
Amesema pamoja na uwepo wa changamoto ya kutoendelea kwa ufadhili wa mradi wa USAID Lishe Project Kigoma, amewataka wataalam kutekeleza afua za lishe kuendana na bajeti walizopanga.
Dkt. Damas Kayera ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amesema lengo la kuboresha lishe ni muhimunkwa kuwa mkoa bado unachangamoto ya uwepo wa utapiamlo.
Nyenzo hizo za usafiri zimetolewa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia Wizara ya Afya, mara baada ya Mkataba wa ufadhili kupitia Mradi wa USAID, Lishe Project Kigoma kufikia tamati, ambapo katika mgao huo gari moja litatumika kusimamia uratibu wa Shughuli za lishe kimkoa na lingine katika Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa