Serikali kupitia Wizara ya Afya imeendelea na Mpango wa kudhibiti na kutoa Tiba kinga dhidi ya Maradhi mbalimbali ambayo yamekuwa yakisababisha vifo, Ulemavu, kupunguza nguvu ya taifa na hata kusababisha serikali kutumia kiwango kikubwa cha fedha.
Kutokana na kuwepo kwa mlipuko wa uginjwa wa polio kwenye nchi jirani zinazopakana na mkoa wa Kigoma, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kudhibiti kuenea kwa maradhi hapa nchini.
Katika kutekeleza Afua hizo muhimu, Mkoa wa Kigoma kupitia Idara ya Afya unatekeleza zoezi la uhamasishaji na utoaji wa chanjo sambamba na utoaji dozi ya nyongeza wa chanjo ya Sindano ya Polio (IPV2)
Ifahamike kuwa, virusi vya ugonjwa wa polio humpata mtu akiwa na umri wowote japo watoto ni kundi linaloathiriwa Zaidi. Maradhi hayo huingia kwa binadamu kupitia chakula kilichochafuliwa kasha huweka makao yao katika utumbo wa mgonjwa na kasha hushambulia midhipa ya fahamu na kusababisha hali ya kupooza kwa sehemu moja au zaidi katika mwili.
Jamii inapaswa kufahamu uwepo wa dalili za ugonjwa wa polio ili kuchukua hatua za kimatibabu mapema ikiwa ni pamoja na motto kukakamaa shingo na mgongo, kuumwa kwa miguu na mikono, homa, kuhara na kutapika na hali inapozidi kuwa mbaya husababisha hali ya kupooza kwa eneo moja au Zaidi katika mwili.
Ili kukabiliana na hali hiyo, serikali kwa muda mrefu imekuwa ikiendesha mazoezi ya utoaji wa kinga kuanzia watoto wanapozaliwa hadi kufikisha umri wa miezi sita, miaka 10 au 14 kutokana na aina ya chanjo.
Ili kudumisha usalama wa watoto, Dkt. Damas Kayera ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma anasema watoto wote wanastahili kupatiwa dozi ya pili ya chanjo ya polio wanapofikisha umri wa miezi tisa. Amesisitiza kuwa, kuanzia mwezi Mei 2025, chanjo ya polio ya IPV2 inatolewa kwa dozi mbili sambamba na chanjo nyingine kwa ratiba inayotolewa na wataalam wa Afya katika vituo vya kutolea huduma.
Upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma anasisitiza kuwa, jamii inapaswa kuzingatia utolewaji wa chanjo hizo ili kuimarisha kinga za watoto dhidi ya magonjwa, kupunguza vifo na ulemavu utokanao na polio sambamba na kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa