• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

MRADI WA UHIFADHI MAZINGIRA WAZINDULIWA KIGOMA

Posted on: May 15th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amezindua mradi wa kujenga  Ustahimilivu wa Mabadiliko ya Hali ya Tabia Nchi mkoani hapa, akimwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mha. Yusuf Masauni.

Uzinduzi huo umefanyika leo Mei 15, 2025 katika Hoteli ya Lake Tanganyika iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji, ambapo mradi huo unalenga kukabiliana na changamoto za athari za kimazingira mkoani hapa kupitia urejeshwaji wa misitu kwa kupanda miti katika maeneo yaliyoathiriwa na ukataji holela wa miti na uharibifu wa mazingira.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Andengenye amesema mkoa unahifadhi zaidi ya wakimbizi 1900,000 kutoka nchi jirani za Burundi na Congo DR, kutokana na kutoimarika kwa hali ya utulivu na amani ambapo katika maeneo wanayoishi kumeshuhudiwa uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwemo ukataji miti kwa ajili ya nishati, kuandaa maeneo ya kilimo na shughuli nyinginezo za kibinadamu.Ameutaja mradi huo kuwa na manufaa makubwa katika matumizi bora ya Ardhi, uhimilivu wa mazingira kwa viumbe hai, kurejesha mfumo wa kiikolojia, usawa wa kijinsia katika muktadha wa kimazingira pamoja na kuendeleza sera ya Taifa katika uhifadhi wa mazingira.

Kupitia hotuba yake, kwaniaba ya waziri Masauni, Andengenye ameushukuru uongozi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa(UNEP) pamoja na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa kuendelea kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwezesha na kufanikisha mradi huo unaoratibu shughuli za uhifadhi wa Mazingira kwa manufaa ya mkoa wa Kigoma na nchi kwa ujumla.

Kamilembe  Mutasa Mkurugenzi  wa Mazingira  Ofisi ya Makamu wa Rais wa Rais (Muungano na Mazingira) amesema mradi huo wenye Thamani ya Shilingi Bil. 54 unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha Miaka mitano(5) katika wilaya za Kasulu, Kibondo na Kakonko.

Amesema Kigoma ni mkoa unaokabiliwa na athari kubwa za uharibifu wa Mazingira ambazo zinazochangiwa na shughuli za kibinadamu haswa katika maeneo yanayohifadhi wakimbizi.Amezitaja athari zinazotokana na mabadiliko ya tabia nchi kuwa ni pamoja na ongezeko la mvua, hali joto, mafuriko pamoja na ukame.

Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • RC ANDENGENYE AZINDUA RASMI ZOEZI LA UGAWAJI VYANDARUA KIMKOA

    May 27, 2025
  • JAMII INAPASWA KUZINGATIA CHANJO KUJILINDA NA MARADHI

    May 20, 2025
  • MRADI WA UHIFADHI MAZINGIRA WAZINDULIWA KIGOMA

    May 15, 2025
  • RC ANDENGENYE AKABIDHI VITENGO VITENGO VYA LISHE MKOA NA WILAYA UVINZA

    May 09, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa