• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

RC ANDENGENYE AZINDUA KAMBI YA MADAKTARI BINGWA WA DKT. SAMIA

Posted on: June 10th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amewataka wakazi mkoani hapa kujenga tabia ya kuchukua tahadhari dhidi ya maradhi mbalimbali kwa kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalam wa Afya  ili kujikinga na kuepukana magonjwa yanayozuilika.

Wito huo umetolewa na Mkuu huyo wa mkoa alipozungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Kambi ya Matibabu ya Madaktari bingwa wa Dkt. Samia kwa ajili ya kutoa huduma kwa ngazi ya Halmashauri, uliofanyika katika Hospitali ya Manispaa ya Kigoma Ujiji na kuitaka jamii kuzingangatia usafi wa watu binafsi na Mazingira yao  ili kujiepusha na kupunguza athari za Magonjwa.

Amesema pamoja na Serikali kuendelea kufanya kazi kubwa ya kusogeza huduma za kiafya kwa wananchi, kila kila mmoja anapaswa kuchukua hatua ya kujikinga dhidi ya maradhi hayo jambo litakalopuguza idadi ya wagonjwa na athari zake katika jamii.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amewakumbusha wakazi kuzingatia ulaji wa mlo kamili ili kupunguza kiwango cha udumavu na utapiamlo kwa watoto kutokana na mkoa kuzalisha chakula  cha kutosha.

Awali akimkaribisha Mkuu wa Kigoma Kaimu Katibu Tawala Mkoa Elisante Mbwilo amewataka wananchi waliojitokeza kupata huduma kupitia madaktari hao kuwa mabalozi kwa kuwafikishia taarifa wahitaji wengine wa huduma hizo waliopo katika maeneo yao.

‘‘Hakikisheni mnawafikishia wengine taarifa kuhusu uwepo wa huduma hii ili waweze kufahamu na kujitokeza kupata matibabu kwa urahisi na ukaribu’’ amesisitiza Mbwilo.

Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Cephlen Budodi amesema mpaka kufikia Mei 10, 2024 jumla ya mikoa 17 imefikiwa huku zoezi hilo likiwa ni endelevu lililenga kuzifikia Halmashauri zote 184 za Tanzania bara.

Budodi ametoa wito kwa wananchi kufika katika hospitali za wilaya ili kukutana na wataaalam hao ikiwa ni fursa muhimu na adhimu ya kupata huduma hizo katika maeneo yao ya karibu.

Upande Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dkt. Jesca Lebba amesema jumla ya madaktari bingwa 40 wamepokelewa mkoani humo kwa ajili ya kutoa huduma bobezi za kitabibu katika Hospitali za wilaya zilizopo kwenye Halmashauri nane za Mkoa wa Kigoma.

Amezitaja huduma zitakazotolewa kuwa ni pamoja na matibabu kwa magonjwa ya kina mama na watoto, upasuaji wa aina mbalimbali, magonjwa ya ndani sambamba na utoaji huduma ya kibingwa kwa upande wa usingizi na ganzi.

Dkt. Lebba amefafanua kuwa huduma kutoka kambi hiyo ya madaktari bingwa kimkoa, zimeanza kutolewa Juni 10 hadi 14,2024 na kuwataka wagonjwa kujitokeza ili kutumia fursa hiyo, ikiwa ni muendelezo wa kusogeza huduma hizo kwa wakazi sambamba na kuwaongezea ujuzi madaktari wa ndani wa mkoa.

Jumanne Selemani ambaye ni Mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ameishukuru serikali ya awamu ya Sita  inayoongozwa na Rais Dkt. Samia kwa kuwezesha upatikanaji wa huduma hiyo katika maeneo ya jirani na kuwapunguzia gharama na muda mrefu wa kufuata huduma hizo nje ya Mkoa.


Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • DCP NARCIS MISSAMA AFANYA ZIARA MKOANI KIGOMA

    May 07, 2025
  • JAJI ASINA AKAGUA ZOEZI LA UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI-KIGOMA

    May 03, 2025
  • VYAMA VYA WAFANYAKAZI VISIGEUKE MAHAKAMA ZA KUWAHUKUMU WATUMISHI-RC ANDENGENYE

    May 01, 2025
  • PICHA; MAENDELEO YA UJENZI WA UKUMBI WA DKT. PHILIP MPANGO KATIKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA KIGOMA

    April 30, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa