uta nikuvute iliyojitokeza baina ya Jeshi la Polisi na madereva wa pikipiki ( Boda boda) katika Manispaa ya Kigoma Ujiji imepatiwa Mwarobaini baada ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye kukutana na kutoa maelekezo yaliyolenga kuimarisha utendaji kazi utakaozingatia Utu na Sheria kwa pande mbili hizo.
Akizungumza na madereva wa pikipiki hao kupitia Mkutano uliofanyika katika Ukumbi wa Kanisa la Anglican Mjini Kigoma, Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa watendaji wa Jeshi hilo kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia utu sambamba na usalama wa watu na vyombo wanavyovikamata.
Amesema baadhi ya watendaji katika jeshi hilo wamekuwa wakitumia nguvu kubwana hata kwenda kinyume cha Sheria na miongozo ya kazi zao wanapotekekeza jukumu la kusimamia utendaji kazi wa bodaboda jambo linalozua malalamiko makubwa katika kundi hilo.
"Niwatake mtangulize utoaji wa Elimu ya usalama barabarani, kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ukaguzi wa vyombo hivyo na kuhakikisha ukamataji wenu unakuwa wenye staha na usioweza kuleta madhara kwa waendesha pikipiki" amesisitiza Andengenye.
Aidha katika hatua nyingine, mkuu wa mkoa amewataka bodaboda katika manispaa hiyo na Mkoa kwa ujumla kuhakikisha vyombo vyao havina dosari za kiufundi na makosa ya barabarani kabla ya kuanza kuvitumia kibiashara.
"Serikali haitoweza kumvumilia mvunja Sheria ikiwemo kuendesha pikipiki bila Leseni, kuendesha vyombo vibovu na hata kutozingatia sheria nyinginezo za usalama barabarani sambamba na usafi" amesisitiza Andengenye.
"Nitoe wito kwenu kuhakikisha kila bodaboda anakuwa mlinzi wa mwenzake sambamba na kutoa taarifa mnapobaini uwepo wa jambo lisilo la kawaida katika maeneo yenu sambamba na kumtambua kila mmoja wenu kuhusu uhalali wake wa kuwa katika maeneo yenu ta kazi" amesisitiza Andengenye.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa