Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amewashukuru wadau wa Maendeleo wa Mkoa wa Kigoma ikiwemo mashirika na Taasisi Binafsi zinazofanya shughuli zake mkoani Kigoma kwa kuendelea kuigusa jamii ikiwemo kutoa misaada mbalimbali ya kiutu kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwaondoloea adha wananchi.
Mhe. Andengenye ametoa Kauli hiyo alipozungumza kwenye hafla fupi ya kugawa vifaa vilivyotolewa na Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF) kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaiyosababishwa na mvua nyingi zilizonyesha mkoani Kigoma kati ya Desemba 2023 hadi Aprili 2024 hususani katika Halmashauri za Kigoma Ujiji, Uviza na Kigoma.
Amewataka wakuu wa wilaya za Uvinza, Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji ambazo zimepokea vifaa hivyo kuhakikisha vinawafikia walengwa na kuwanufaisha kama ilivyokusudiwa sambamba na kuwataka wananchi kuepuka kujenga katika maeneo ya mabondeni ili kuepuka athari zitokanazo na mvua jambo linaloweza hatarisha usalama wa maisha na mali zao.
Upande wake Mkuu wa Ofisi ya Shirika la UNICEF Kigoma Justus Ndenzako amesema vifaa vilivyokabidhiwa kwa wakuu wa wilaya hizo kwaniaba ya wahitaji ni pamoja na Magodoro 200, ndoo 300, blangeti 310, vyandarua 100 pamoja na mashuka 10 vyote vikiwa na Thamani ya zaidi ya Shilingi Mil. 20
Amefafanua kuwa, shirika la UNICEF linatoa linaendelea kushirikiana na Serikali katika kutekeleza miradi mbailmbali ya kijamii ikiwemo ile iliyopo katika Sekta zinazohusisha utoaji wa huduma za jamii, hivyo kutoa misaada hiyo ni mojawapo ya sehemu ya utekelezaji wa kazi zinazoguza jamii moja kwa moja.
Mkuu wa wilaya ya Uvinza Mhe. Dinah Mathamani ameushukuru uongozi wa shirika hilo na kuahidi kufikisha misaada hiyo moja kwa moja kwa walengwa.
Hadi kufikia Mwezi Juni 2023 jumla ya Kaya 411 zilithibitika kukosa makazi katika Halamshauri za Uvinza, Kigoma na Manispaa ya Kigoma Ujiji, huku jumla ya wakazi 3,419 waihama makazi yao kutokana na athari za Mvua zilizonyesha mkoani Kigoma.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa