Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amewataka watumishi wa Umma kujenga utamaduni wa kutunza vitendea kazi wanavyotumia katika utendaji kazi wao ili viweze kudumu na kutoa huduma kwa muda mrefu kwa manufaa ya wanaowahudumia na wao wenyewe.
Andengenye ametoa kauli hiyo alipozungumza kwenye hafla fupi ya kukabidhi gari lililotolewa na Serikali kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Kigoma na kuusisitiza uongozi katika mamlaka za Umma mkoani hapa kuhakikisha unasimamia matumizi ya magari sambamba na kuyafanyia matengenezo kwa wakati.
Kuhusu hali ya upatikanaji wa huduma ya Maji katika maeneo ya vijijini, Mkuu huyo wa Mkoa amesema mpaka kufikia mwaka 2024 hali ya upatikanaji wa Maji imefikia Asilimi 74 ambapo kabla ya utekelezaji wa miradi hiyo unaofanywa na Serikali ya awamu ya Sita hali ya upatikanaji wa huduma hiyo ilikuwa Asilimi 54.
Amesema mpaka kufikia mwaka 2025 matarajio ni kufikia Asilimia 85, hali itakayomaliza kwa kiasi kikubwa adha ya upatikanaji wa huduma ya Maji kwa wakazi wa Mkoa wa Kigoma.
Upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa ameahidi kushirikian na wakuu wa Taasisi za Serikali ili kuhakikisha vitendea kazi vilivyopo ikiwemo magari, yanatunzwa na kutumika kwa usahihi ili yaweze kuwarahisishia watendaji kuifikia jamii kwa lengo la kuhakikisha utooaji wa huduma bora kwa wananchi.
Mha. Mathius Mwenda ambaye ni Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Kigoma amesema nyenzo hiyo itawawezesha kuongeza kasi ya ufuatailiaji wa hali ya utoaji wa huduma zinazotolewa na RUWASA mkoani Kigoma.
Amesema kwa sasa hali ya upatikanaji wa maji katika maeneo ya Halmashauri za Wilaya mkoani Kigoma inaridhisha kufuatia maboresho makubwa yanayoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa