Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thpbias Andengenye ameupongeza Uongozi wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT TZ) kwa kutoa ufadhili wa nusu ya ada kwa walimu wa shule za Umma jambo lililochangia kwa kiasi kikubwa kuboresha Taaluma ya watendaji katika kada hiyo.
Kauli hiyo imetolewa na Kiongozi huyo alipohutubia Kongamano la 34 la wanazuoni wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania lililofanyika katika Kituo cha chuo hicho cha Mkoa wa Kigoma kuelekea Mahafali ya 43 ya chuo yanayotarajiwa kufanyika Desemba 5, 2024 mkoani humo.
Kupitia hotuba yake Andengenye amekipongeza chuo hicho kwa kudumisha mahusiano na taasisi za kitaaluma za ndani na nje ya nchi kwa lengo la kubadilishana utaalam, kufanya tafiti pamoja na kuendesha miradi mbalimbali ya pamoja kwa lengo la kuimarisha utoaji wa taaluma kwa wanafunzi wa chuo hicho.
Andengenye amewapongeza wahitimu wote wanaotarajiwa kutunukiwa kutokana na kuhitimu ngazi mbalimbali za kitaaluma na kuwasisitiza kutoishia hatua walizofikia.
Ameongeza kwa kutoa wito kwa wahitimu hususani walio katika mifumo ya kuajiriwa na kujiajiri kwenda kuongeza ufanisi katika utendaji kazi wao ili waweze kujitofautisha na kuwa wahitimu shindani katika soko la ajira.
Prof. Carlolyne Nombo Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu kwa kuendelea kuwekeza katika ngazi zote za kielimu ili kuleta ufanisi katika elimu Msingi, Sekondari na ngazi za vyuo.
Prof. Nombo ameupongeza uongozi wa chuo kwa kuzalisha wataalam wengi na wenye elimu bora, kwani elimu inayotolewa na chuo hicho inawapa fursa wahitimu kuitumia ndani na nje ya nchi na kuleta matokeo chanya.
"Ninaamini kupitia uzoefu wa kutekeleza mfumo wa elimu nyumbuifu mtaelekeza na kutoa ushauri kwa Wizara ya Elimu ili kupata namna ya kutoa elimu kwa utaratibu huo katika ngazi mbalimbali za kielimu nchini" amesema.
Amesisitiza kuwa, Wizara itaendelea kufanya kazi kwa karibu ikiwa kutekeleza miradi ya kimkakati ikiwemo utekelezaji mradi wa HEET unaolenga kuimarisha Utawala, Miundombonu na kujenga misingi ya elimu.
"Mradi wa HEET umejielekeza kujenga maabara ya kisasa ya Sayansi mkoani Kigoma jambo, litakalokuwa fursa kwa wanafunzi wa kituo cha Kigoma na maeneo jirani kusoma kwa vitendo zaidi" amesisituza Prof. Nombo.
Aidha ameusisitiza uongozi wa mkoa kufanya ufuatiliaji wa karibu ili kuhakikisha ujenzi wa Maabara hiyo unakamilika ndani ya muda uliopangwa.
Niwaahidi wizara kufanya kazi kwa karibu ili kuhakikisha dhamira ya Chuo Kikuu Huria ya kutoa elimu kwa njia ya masafa ikiwemo elimu ya juu inaendelea kufanyika kwa ufasaha.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa