Wakazi katika vijiji vya Chankele na Bubango wilayani Kigoma wametakiwa kuepuka kufanya shughuli za kibinadamu jirani na vyanzo vya Maji sambamba na kutunza miundombinu ya Maji iliyopo ili kuwapunguzia adha ya upatikanaji wa huduma hiyo.
Wito huo umetolewa kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye kufanya ziara ya ukaguzi wa Miundombinu ya Maji wilayani humo na kusisitiza kwamba kila mtu anajukumu la kulinda vyanzo vya Maji na miundombinu inayowezesha upatikanaji wa huduma hiyo.
‘‘Niwaambie ukweli waathirika wakubwa wa ukosefu wa huduma ya maji ni wanawake kwani hujikuta wakitumia muda mwingi kutafuta maji kwenye mito na visima na kusababisha kukosa muda wa kutosha wa kushiriki shughuli za uzalishaji mali pamoja na kuhudumia familia zao’’ amesema Mkuu wa Mkoa.
Amesema ili kuhakikisha chanzo hicho kinakuwa salama, Andengenye amewaelekeza watendaji watendaji wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) kushirikiana na wananchi kuhakikisha hakuna shughuli yoyote ya kibinadamu zinazofanyika katika maeneo ya vyanzo vya maji wilayani humo.
Amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais. Dkt. Samia Suluhu ni kuhakikisha tunamtua mama ndoo kichwani na kuondokana na uchotaji wa maji wa kwenye magati, visima au mitoni bali kuhakikisha kila kaya inapata huduma hiyo.
Chanzo cha Maji cha Bubango-Chankele kimerekebishwa kwa kupanuliwa kwa gharama ya shilingi Milioni 900 ambapo kinahudumia watu zaidi ya 900 ambao ni wakazi katika maeneo hayo ambapo jumla ya magati 16 yamejengwa katika kijiji cha Chankele na 19 katika kijiji cha Bubango.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255738192977
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa