Umoja wa Ulaya kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) wamezindua mradi wa pamoja wa kuvuka mpaka wenye lengo la kuendeleza ulinzi na ustahimilivu kwa Wakimbizi wa Burundi waliopo nchini Tanzania sambamba na kuboresha huduma kwa wale wanaorejea nchini humo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo katika Kambi ya Wakimbizi ya Nyarugusu ikiyopo wilayani Kasulu, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye ameusisitiza uongozi wa serikali ya Burundi kuboresha huduma za kijamii na fursa za kiuchumi kwa waliorejea nchini humo jambo ambalo litahamasisha wakimbizi wengi wa Burundi kurejea nyumbani ikiwa ni pamoja na kuongeza fedha za kujikimu kwa wale wanaorejea kwa hiyari.
Christine Grau ambaaye ni balozi wa Ulaya nchini, amesema wataendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kuhakikisha wakimbizi wanaorejea nchini burundi wanaishi maisha bora na yenye usalama.
Upande wake Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Burundi Elizabetta Pietrobonamesema kupitia mradi huo ukioanza kutekelezwa Oktoba 2023 wenye Thamani ya fedha za Ulaya (Euro) Mil.40 wakimbizi wa Burundi wanawezeshwa kupata vitambulisho vya uraia, vyeti vya kuzaliwa, vya elimu na vile vya ndoa.
Ili kuhakikisha kufikia malengo ya kudumu katika zoezi la urejeaji kwa wakimbizi hao nchini Burundi, Mkurugenzi wa huduma za wakimbizi Sudi Mwakibasi amesema wanauomba Umoja wa Ulaya na serikali ya Burundi kuendelea kuunga mkono mpango huo wa urejeaji wa hiyari ili kuhakikisha wakimbizi wote wanarejea nchini humo.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa