• Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko / Mrejesho |
KIGOMA   REGION
KIGOMA   REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Kigoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo
    • Seksheni
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Seksheni ya Elimu
      • Seksheni ya Afya
      • Seksheni ya Miundombinu
      • Seksheni ya Serikali za Mitaa
      • Seksheni ya Mipango na Uratibu
      • Seksheni ya Uchumi na Uzalishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Fedha
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwami
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo cha Manunuzi na Ugavi
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Kibondo
      • Halmashauri ya Kibondo
    • Wilaya ya Kigoma
      • Halmashauri ya Kigoma
      • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Wilaya ya Kakonko
      • Halmashauri ya Kakonko
    • Wilaya ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu
      • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Wilaya ya Uvinza
      • Halmashauri ya Uvinza
    • Wilaya ya Buhigwe
      • Halmashauri ya Buhigwe
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Kigoma Ujiji
    • Halmashauri ya Buhigwe
    • Halmashauri ya Kasulu
    • Halmashauri ya Kasulu Mji
    • Halmashauri ya Kibondo
    • Halmashauri ya Uvinza
    • Halmashauri ya Kakonko
    • Halmashauri ya Kigoma
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Kigoma Special Economic Zone
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mikakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba za Viongozi
    • Picha

RC ANDENGENYE AFUNGUA SOKO LA KIMKAKATI MNANILA BUHIGWE

Posted on: October 12th, 2023

MKUU WA MKOA WA KIGOMA KAMISHNA JENERALI MSTAAFU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI THOBIAS ANDENGENYE AKIZUNGUMZA NA WAKAZI WA KIJIJI CHA MNANILA(HAWAPO PICHANI) KILICHOPO WILAYANI BUHIGWE MARA BAADA YA KUFUNGUA SOKO LA KIMKAKATI MNANILA WILAYANI HUMO.

RC ANDENGENYE AKIJIANDAA KUKATA UTEPE KUASHIRIA UFUNGUZI RASMI WA SOKO LA KIMKAKATI MNANILA.MWONEKANO WA SOKO LA KIMKAKATI MNANILA.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amefungua Soko la kimkakati Mnanila  lililopo Kata ya Mnanila wilayani Buhigwe mkoani hapa.

Ufunguzi wa Soko hilo lililojengwa kwa Thamani ya Shilingi Bil.2.5 fedha kutoka Serikali Kuu, umefanyika Leo  Oktoba 12, 2023 huku ukienda sambamba na  ziara ya Mkuu huyo wa mkoa iliyolenga kukagua miradi maendeleo na kusikiliza kero za wananchi wilayani humo.

Akizungumza na wakazi waliojitokeza kwenye ufunguzi wa Soko hilo lililopo mpakani mwa Tanzania na Burundi, Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wanufaika wa mradi huo kuitumia vizuri fursa hiyo kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi.

Aidha, katika kukabiliana na changamoto za uendeshaji wa Soko hilo,  Andengenye ameuelekeza uongozi wa soko kuzingatia uwazi na ushirikishwaji ili kuondoa malalamiko mbalimbali yanayojitokeza miongoni mwa wafanyabiashara.

Amewasisitiza wafanyabishara hao kuendelea kuchangia  makusanyo ili kuiwezesha Serikali kuendelea kulipanua pamoja na kulifanyia maboresho soko hilo ili kuiwezesha serikali kufanya maboresho ikiwemo upanuzi wa miundombinu na kutoa fursa ya ongezeko la wafanyabiashara katika eneo hilo.

Akiwasilisha Taarifa ya Maendeleo ya Soko hilo, Kaimu Mkuu wa Sehemu ya Viwanda na Biashara Halmashauri ya Buhigwe Onesphory John amesema ujenzi wa Soko hilo umelenga kuwakutanisha wafanyabiashara kutoka nchi zote mbili ili kuongeza chachu ya ukuaji wa biashara katika eneo hilo.

Amefafanua kuwa jumla ya vibanda 144 vimekamilika na tayari wafanyabishara mia moja wamekamilisha taratibu zinazohusiana na zabuni za upangishaji na kupatiwa vibanda hivyo.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Mkoa ameiasa jamii kujenga utamaduni wa kupima Afya ili kuepukana na usugu wa maradhi unaosababaisha baadhi yao  kujiingiza katika Imani za kishirikina ikiwemo Ramli chonganishi kufuatia kuugua kwa muda mrefu.

‘’Jengeni tabia ya kupima Afya mara kwa mara na ili mkibainika na matatizo ya kiafya muweze kupata matibabu badala ya kutuhumiana kuhusu Imani za kishirikina na kukimbilia kwa kina kamchape, hao ni matapeli  achaneni nao’’ amesisitiza.

Aidha Mkuu wa Mkoa ametumia ziara hiyo ya kikazi kusikiliza kero mbalimbali za wakazi wa Buhigwe na kutatua, kushauri na kuwaelekeza namna bora ya kutafuta suluhisho la kudumu la changamoto hizo.

Pia Mkuu huyo wa Mkoa amewasisitiza wakazi wilayani humo kutunza Mazingira kwa kupanda miti rafiki kwa vyanzo vya maji ili kuendelea kuutunza mto Malagarasi ambao ni chanzo kikuu cha ziwa Tanganyika.


Matangazo

  • MAZOEZI KWA AFYA YAKO March 23, 2017
  • UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA 2024 September 12, 2024
  • UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KIGOMA November 12, 2018
  • Fomu ya Usajili wa Maonesho TBS Kigoma May 01, 2022
  • Ona vyote

Habari Mpya

  • JESHI LA UHAMIAJI KIGOMA LAPONGEZWA KATIKA KUKABILIANA NA WAHAMIAJI HARAMU

    June 23, 2025
  • MRADI WA BARABARA MWANDIGA KAGUNGA AWAMU YA KWANZA WAFIKIA 95%

    June 21, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA WAANZA KAMBI YA MATIBABU KIGOMA

    June 16, 2025
  • MRADI WA UHIFADHI MAZINGIRA WAZINDULIWA KIGOMA

    May 15, 2025
  • Ona vyote

Video

RC ahimiza wananchi anuani za Makazi
Video nyingine

Tovuti zinazo fanana

  • HALMASHAURI YA WILAYA YA BUHIGWE
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KASULU
  • HALMASHAURI YA MJI KASULU
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIBONDO
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA KIGOMA
  • HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGOMA UJIJI
  • HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA

Tovuti zinazo husiana

  • TAMISEMI
  • UTUMISHI PORTAL
  • IKULU
  • OFISI YA TAKWIMU YA TAIFA
  • IDARA YA HABARI MAELEZO
  • TOVUTI KUU YA SERIKALI

World visitors tracker

world map hits counter

Wasiliana Nasi

    MKOA WA KIGOMA

    Anuani: S.L.P 125

    Simu: 0282802330

    Simu ya kiganjani: +255766853404

    Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz

Other Contacts

   

Visitors Counter

https://bachelorthesiswritingservice.com

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa