Katika kuhakikisha Halmashauri mkoani hapa zinapata ufumbuzi wa kudumu dhidi ya hoja mbalimbali za Ukaguzi wa Hesabu za Serikali zinazojitokeza na ambazo zinaweza kuepukika, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye ameuagiza Uongozi katika Halmashauri za Mkoa wa Kigoma kuboresha Mfumo wa utunzaji wa nyaraka zikiwemo Hati za malipo ya Fedha ili kurahisisha upatikanaji wake pale zinapohitajika kwa ajili ya kujibu hoja hizo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa amewaelekeza wakuu wa Vitengo vya Fedha na Biashara pamoja na Ugavi kutoa ushirkiano wa karibu kwa wakaguzi wa ndani katika Halmashauri ili kubaini Hoja hizo mapema na kuzitafuatia Ufumbuzi kwa pamoja.
Juni 13, 2023 Mkuu wa Mkoa amefungua na kushiriki Mikutano ya Mabaraza Maalum ya kupokea na kujadili Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 katika Halmashauri ya Mji na Wilaya Kasulu.
Kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 Halmashauri hizo zimefanikiwa kupata Hati Safi ya Ukaguzi wa Hesabu.
MKUU WA MKOA WA KIGOMA MHE. THOBIAS ANDNGENYE AKIZUNGUMZA NA WAH. MADIWANI KATIKA MKUTANO MAALUM WA BARAZA LA MADIWANI(CAG) KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU JUNI 13, 2023 KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU.
KATIBU TAWALA WA MKOA WA KIGOMA MHE. ALBERT MSOVELA AKIZUNGUMZA NA WAH. MADIWANI (HAWAPO PICHANI) KWENYE MKUTANO MAALUM WA BARAZA LA MADIWANI (CAG) KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU JUNI 13, 2023
MKUU WA MKOA WA KIGOMA (KULIA) AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA KATIBU TAWALA MKOA ALBERT MSOVELA, WAKIFUATILIA TAARIFA YA MKAGUZI NA MDHIBITI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI KATIKA HALMASHAURI YAMJI KASULU KWA MWAKA 2021/2022
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa