Serikali mkoani Kigoma imeahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya nchi ya Burundi ili kudumisha Amani na maendeleo ya kiuchumi kwa lengo la kuboresha maisha ya wakazi katika nchi hizo mbili.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma alipofungua kikao cha wataalam wa uimarishaji mpaka wa kimataifa wa Tanzania na Burundi kilichofanyika katika Hoteli ya Sunset Vista iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani hapa.
Amesema ili kuinua uchumi wa mataifa hayo, viongozi wa pande mbili hizo wanaendelea kuimarisha sekta ya Uchumi kwa kufanya maboresho ya miundombinu ya uchukuzi itakayozidi kuziunganisha Tanzania na Burundi kibiashara.
Aidha, Kiongozi huyo amewataka wajumbe wa kikao hicho kuandaa mpangokazi utakaokuwa dira katika kusimamia na kuimarisha mpaka baina ya nchi hizo mbili.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa