Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye(Kulia) akifafanua Jambo mbele ya Mkuu wa Misheni wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) Maurizio Busatti pamoja na Ujumbe alioongozana nao.
Mkuu wa Mkoa Mhe. Thobias Andengenye akiwa katika Picha ya pamoja na Maurizio Busatti (watatu kutoka kulia) pamoja na Baadhi ya watumishi wa Shirika la IOM.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye akwa katika picha ya Pamoja na Maurizio Busatti mara baada ya mazungumzo baina yao yaliyofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo Tarehe 23 Septemba 2022.
Mkuu wa Misheni wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) Maurizio Busatti Leo Tarehe 23, Septemba 2022, amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma CGF(Mst) Thobias Andengenye Ofisini kwake ambapo wawili hao wamekubaliana kuendelea kuimarisha ushirikiano katika Nyanja zinazozigusa Taasisi zao ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mkuu huyo wa Misheni, amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kuwa, Shirika hilo litaendelea kutoa Ushirikiano kwa Serikali katika kuwahudumia wakimbizi waliopo nchini pamoja na kutoa misaada katika nyanja za Elimu na Afya kwa Jamii inayozunguuka Kambi za wakimbizi mkoani hapa.
Naye Mkuu wa Mkoa , amemshukuru Mkuu huyo wa Misheni wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji kwa kufika mkoani hapa ikiwa ni sehemu muhimu kwake kujionea hali halisi ya utendaji wa Shirika hilo lisilo la kiserikali na kuahidi kuendelea kumpa ushirikianopale itakapohitakika kufanya hivyo.
''Shughuli mnazozifanya kwa Jamii yetu mkoani hapa zinatupa Ari na shauku ya kuendelea kushirikiana nanyi kwa maslahi ya mapana ya wananchi ambapo huduma zenu zimendelea kuwaimarisha katikakuboresha maisha yao na ujenzi wa Taifa kwa ujumla'' alisema Andengenye.
Aidha aliishikuru Taasisi hiyo isiyo ya kiserikali kwa misaada wanayoendelea kuitoa kwa jamii inayozunguuka Kambi hizo ikiwemo ile ya kielimu na Afya.
Mkoa wa Kigoma una Jumla ya Kambi mbili za wakimbizi ambazo ni Kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu yenye wakimbizi kutoka nchi za Burundi na Congo pamoja na Kambi ya Nduta katika wilaya ya Kibondo yenye wakimbizi kutoka nchi ya Burundi pekee.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa