OPERESHENI ONDOA MIFUGO KUTOKA NJE YA NCHI KUFANYIKA MIKOA 12 KWA SIKU 15 NCHINI
Posted on: October 27th, 2017
Wizara ya Mifugo na Uvuvi imetangaza kufanya operesheni kabambe ya siku 15 ya kuondoa mifugo yote inayotoka nchi za jirani katika mikoa 12 iliyopo mipakani hapa nchini.
Akizungumza katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Waziri mwenye dhamana na mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina(MB) amesema wizara yake imejipanga kuondoa mifugo yote ambayo si ya nchi hii ndani ya siku 15 ambapo yeye pamoja na Msaidizi wan a Katibu Mkuu wamegawana kusimamia zoezi ilo kwa siku 15.
Ametaja mikoa itakaofikwa na zoezi hilo ni Kigoma, Kagera, Katavi, Kilimanjaro, Arusha na Mara, mikoa mingine ni pamoja na Songwe, Njombe, mbeya
Mhe. Mpina amesema asilimia 30 ya malisho ya Mifugo hapa Tanzania yanatumiwa na mifugo ya wafugaji toka nje ya nchi, jambo linalofanya wafugaji wa ndani kukosa malisho na ardhi ya kulima na hivyo kusababisha migogoro mingi kati ya wafugaji na wakaulima
Sambamba na kuzuia migogoro inayosababishwa na mifugo hiyo amesema kuwa wizara itaweza kudhibiti magonjwa ya mifugo yanayoweza kusababishwa na mifugo inayoingizwa nchinikutoka nchijirani kwa kufuata malisho.
“udhibiti wa mifugo utasaidia pia kuepukahasara kwa serikali na wafugaji wetu kupteza mifugo yao sababu ya magonjwa, na uchafuzi wa mazingira, zoezi hili ni kwa mujibu wa sharia ya Mifugo Na. 17 ya mwaka 2013.
Imeelezwa kuwa hatua kali itachukuliwa kwa mifugo hiyo ikipatikana ikiwemo faini au kutaifishwa kwa mifugo, amewataka watu walioingiza mifugo nchini kinyemela kuiondoa maramoja kabla ya kupatwa na dhahama hiyo.
Ameagiza kuwa baada ya siku 15 za operesheni kila Mkoa utahakikisha kutoa taarifa za uthibitisho wa kutoingia Mifugo tena kutoka nchi jirani. Aidha, Mhe. Mpina ameagiza Mikoa yote kukamilisha zoezi la upigaji chapa mifugo kukamilika ifikapo tarehe 30 Desemba, 2017
Aye Mkuu wa Mkoa amemhakikishia Waziri kuwa Mkoa upo taari kuhakikisha zoezi la kuondoa mifugo kutoka nje linafannikiwa kwani kumekuwepo na kero ya uingizwaji wa mifugo kutoka Burundi na Rwanda Mkoani humo.