Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo unaofanywa mkoani Kigoma unapaswa kwenda sambamba na ukusanyaji wa mapato ili kukuza uchumi wa Mkoa na Taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na Rais Samia, wakati akihutubia maelfu ya wananchi wa Mkoa wa Kigoma waliojitokeza katika uwanja wa Lake Tanganyika, mara baada ya kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya Siku Tatu mkoani hapa.
‘’Kukamilika kwa Miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa Barabara ya Kabingo hadi Manyovu itakayounganisha mkoa na Nchi ya Burundi, kunapaswa kuendana na ongezeko la ukusanyaji wa mapato na kukuza uili kuchochea mabadiliko ya kimaendeleo mkoani hapa’’amesema.
‘’Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya usafirshaji, upatikanaji wa Umeme wa uhakika, vitumike katika kuimarisha uchumi wa wanakigoma na watanzania kwa ujumla’’amesema Mhe. Rais Samia.
Kupitia ziara yake hiyo, Mhe. Rais, sambamba na kuongea na wananchi katika meneo aliyopita, ameweka mawe ya Msingi katika Miradi ya Barabara Manyovu hadi Kabingo/Kakonko, Barabara ya Kibondo-Nduta, Bandari ndogo ya Kibirizi pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Maweni-Kigoma.
Aidha Mhe. Rais amefungua Hospitali ya wilaya ya Kakonko, Mradi wa Maji Kinyamfisi uliopo Kakonko Mjini, Barabara ya Kabingo-Nyakanazi, Chuo cha Ualimu Kasulu pamoja na Ofisi ya Mkuu wa wilaya Buhigwe.
Pia Mhe. Rais, amezindua mradi wa Umeme wa gridi ya Taifa wa Megawati 20 na kuzima majenereta ambayo hapo awali yalikua yakizalisha kiasi cha Megawati 14 kwa Mkoa Mzima.
Rais samia amehitimisha ziara yake mkoani Kigoma siku ya Leo Tarehe 18 Oktoba 2022.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa