Ubalozi wa Kifalme wa Norway leo umetanganza kuingia makubaliano na Umoja wa Mataifa nchini Tanzania ambapo Norway itachangia Dola za Marekani milioni 4.3 (takribani Shilingi bilioni 9.9) kwa Umoja wa Mataifa ili kusaidia utekelezaji wa Programu ya Pamoja ya Kigoma (KJP). KJP ni programu ya kieneo inayotekelezwa kwa ushirikiano wa Mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na serikali za mkoa na wilaya kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo katika jamii za Mkoa wa Kigoma ambazo hivi sasa zinawahifadhi takribani wakimbizi na waomba hifadhi 278,000.
Programu ya Pamoja ya Kigoma (KJP) ni mradi wa kieneo unaoshughulikia sekta mtambuka kwa lengo la kuimarisha maendeleo na usalama wa watu wa Mkoa wa Kigoma. Programu hiyo inahusisha mashirika 16 ya Umoja wa Mataifa na ulianzishwa kwa kushirikiana na Serikali ya mkoa na zile za wilaya kwa kuzingatia mahitaji ya maendeleo ya Kigoma na uwezo wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania. Mashirika hayo 16 ya Umoja wa Mataifa yanashirikiana katika maeneo 7 ambayo ni Nishati na Mazingira Endelevu; Uwezeshaji Vijana na Wanawake Kiuchumi; Kukomesha Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto; Elimu inayowalenga wasichana na wasichana waliobalehe; Usafi wa Maji na Mazingira (WASH); na Kilimo; na, Afya, VVU na Lishe.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa