Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ameendelea na ziara yake mkoani hapa ambapo akiwa njiani kwenda wilayani Kasulu amepata fursa ya kusikiliza kero kisha kuzungumza na wakazi wa Kata ya Mwandiga kisha kumuelekeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuhakikisha unafanyika ujenzi wa Kituo cha Polisi na kusisitiza kuwa kituo hicho kikamilike Ifikapo Oktoba 2025.
Aidha amemuelekeza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI kupitia kwa Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Zainab Katimba kuhakikisha ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kata ya Mwandiga unafanyika na kukamilika ifikapo Oktoba 2025.
Sambamba na Maagizo hayo, Katibu Mkuu amesisistiza kuendelea kwa kasi kazi ya usambazaji wa Huduma ya Maji na Umeme katika Halmashauri ya Kigoma vijijini ili kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo muhimu kwa wananchi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa