Naibu Waziri wa Uchukuzi Mhe. Atupele Mwakibete (Mb) yupo katika ziara ya Kikazi mkoani hapa kwa Lengo la Kukagua Maendeleo ya Ujenzi na uboreshaji wa Miundombinu ya Uchukuzi.
Akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma alipomtembelea Ofisini kwake leo Tarehe 17 Agosti 2022, amesema lengo la Ziara hiyo ya Siku Tatu ni kukagua maendeleo ya Ujenzi wa Meli pamoja na kutembelea Shirika la Reli na kukagua Uwanja wa Ndege wa Mkoa.
Amesisitiza kuwa, Mkoa wa Kigoma unachangamoto ya ukosefu miundombinu ya usafirishaji kwa njia ya Maji, tatizo la chakavu wa Reli pamoja na uwepo wa Uwanja wa ndege usiokidhi vigezo vya kupokea ndege kubwa kwa ajili ya kusafirisha abiria na mizigo.
‘’Serikali Chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imejielekeza katika kuhakikisha inaboresha Miundombinu ya usafirishaji ili kukuza na kuinua uchumi kwa lengo la upatikanaji wa Maendeleo ya Wananchi na Taifa kwa ujumla’’
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, amemshukuru Naibu Waziri kwa Ujio wake huku akitanabaisha kuwa, ziara hiyo itaongeza msukumo wa utendaji kazi kwenye miradi ya uchukuzi inayoendelea kutekelezwa.
Aidha, amememshuku kwa ziara anayoifanya kwani itamsaidia kubaini changamoto mbalimbalizinazoendelea kujitokeza katika baadhi ya miradi inayoendelea kutekelezwa na ile inayotumika.
Naibu Waziri Waziri anatarajia kutembelea Mamlaka ya Viwanja vya ndege kwa kukagua uwanja wa ndege wa Kigoma, Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari na Shirika la Reli Tanzania mkoani hapa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa