Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uwakala wa Meli Nchini (TASAC) Capt. Musa Mandia amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye Ofisini kwake Leo Tarehe 11, Oktoba 2022, ambapo wawili hao wamezungumzia Dhamira ya Shirika hilo kutembelea na kutambua maeneo yatakayofaa kuanzishwa kwa vituo vya uokoaji katika Ziwa Tanganyika.
Capt. Mandia amesema ujio wake mkoani hapa, unadhamira kutekeleza maagizo ya Serikali ya kujenga vituo cha Uokoaji katika Ziwa Tanganyika mkoani Kigoma huku akibainisha kuwa, kazi za vituo hivyo zitakuwa ni kubaini na kutoa tahadhari ya uwepo wa Hali ya Hewa hatarishi ziwani, kutambua pamoja na kuwahi kufanya shughuli za uokozi inapotokea ajali katika maeneo ya Maji.
Naye Mkuu wa Mkoa Mhe. Andengenye, amesema ujenzi wa vituo hivyo utasaidia kuimarisha usalama wa abiria na mali zao.
‘‘Tumeshuhudia ajali mara kadhaa zikipoteza maisha ya watu na mali katika ziwa Tanganyika hivyo tunaimani kukamilika kwa mradi wenu kutaimarisha usalama pamoja na kutoa misaada ya haraka kwa matukio ya dharura yatakayojitokeza katika ziwa Tanganyika’’ amesema.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa