MKUU WA MKOA WA KAGERA MHE. FATMA MWASSA AKIMKABIDHI MWENGE WA UHURU MKUU WA MKOA WA KIGOMA KAMISHNA JENERALI MSTAAFU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MHE. THOBIAS ANDENGENYE. MAPOKEZI HAYO YAMEFANYIKA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO LEO AGOSTI 16, 2023.
MKUU WA MKOA WA KIGOMA KAMISHNA JENERALI MSTAAFU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MHE. THOBIAS ANDENGENYE(KULIA) AKIMKABIDHI MWENGE WA UHURU MKUU WA WILAYA YA KAKONKO KANALI MICHAEL MASALA KWA AJILI YA KUANZA MBIO ZA MWENGE WA UHURU KATIKA WILAYA YA KAKONKO.
Mwenge wa Uhuru umeanza Mbio zake Mkoani Kigoma Leo Agosti 16,2023 ukitokea Mkoani Kagera, ambapo ukiwa mkoani hapa utatembelea, kukagua pamoja na kuweka mawe ya Msingi kwenye Miradi mbalimbali yenye Thamani ya zaidi ya Shilingi Bil.18.3 katika Halmashauri nane za Mkoa.
Awali akipokea Mwenge huo katika Wilaya ya Kakonko, Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema Miradi 21 inatarajia kuzinduliwa, mitatu kufunguliwa, 19 kuwekewa mawe ya Msingi pamoja na kutembelea miradi 21 huku mingine miwili ikiwa ni ugawaji wa vyombo vya usafiri pamoja na vyakula kwa waathirika wa Virusi vya UKIMWI.
Andengenye amesema miradi hiyo itazihusu Sekta za Huduma za Jamii, Ujenzi wa majengo ya Serikali pamoja na Miundombinu ya Barabara, Kilimo, Uhifadhi wa Mazingira pamoja na uwezeshaji kiuchumi kwa vikundi vya Vijana, wanawake na watoto.
Ameendelea kusisitiza kuwa, Mwenge wa Uhuru ni kichocheo muhimu cha Maendeleo nchini na umeendelea kuwa nguzo munimu katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya watanzania kwa kudumisha uwazi, umoja na mshikamano.
Aidha kiongozi huyo wa Mkoa amewataka wasimamizi wa miradikutanguliza uzalendo ili kuhakikisha miradi hiyo inafanyika kwa kiwango bora na kudumu kwa muda mrefu.
Akikagua mradi wa Ujenzi wa Jengo la Nyumba ya Makazi ya Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa Mwaka 2023 Abdallah Kaim, ameonyesha kuridhishwa na utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi huku akisisitiza wasimamizi kuzingatia michoro na viwango vinavyopendekezwa na Serikali katika ujenzi wa miradi.
Amesema kazi zote zinazotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita zimelenga kuboresha maisha ya wananchi hivyo Serikali haitosita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayeonesha utendaji usioridhisha.
Mwenge wa Uhuru umekagua na kuridhishwa na miradi yote ya Maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko pia kiongozi wa mbio hizo amesisitiza kutekelezwa haraka kwa maelekezo aliyoyatoa kwa watendaji kwa lengo la kuondoa dosari ndogo zilizojitokeza katika baadhi ya miradi.
PICHA ZA BAADHI YA MIRADI ILIYOTEMBELEWA NA MBIO ZA MWENGE WA UHURU WILAYANI KAKONKO.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa