Mwenge wa Uhuru 2019, umepokelewa katika Mkoa wa Kigoma ambapo unatarajiwa kukimbizwa takribani kilomita 919 na kutembelea jumla ya Miradi 54 yenye thamani ya shilingi bilioni 10.6.
Aidha, kati ya miradi hiyo, miradi 21 itazinduliwa; miradi 4 itafunguliwa; miradi 16 itawekewa mawe ya msingi; miradi 8 itatembelewa na kukaguliwa; miradi 2 itakuwa ya uwezesho wa vikundi vya wajasiliamali vijana, wanawake na watu wenye ulemavu; miradi 2 ya mapambano dhidi ya malaria; na miradi miwili ni ugawaji wa hatimiliki za kimila.
Vilevile, sehemu ya miradi hiyo ni maeneo ya kumbukumbu ya kazi zilizofanywa na Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.
Katika jumla ya shilingi bilioni 10.6 ambayo ni thamani ya miradi yote 54 itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu 2019, kiasi cha milioni 429.3 sawa na asilimia 4% ni mchango wa nguvu ya wananchi ambapo Serikali Kuu imechangia shilingi bilioni 7.2 sawa na 67.2% wakati 2.3% sawa na shilingi milioni 240.2 ni mchango wa Halmashauri za Mkoa wa Kigoma.
Sambamba na hilo Mchango wa wahisani katika miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni shilingi bilioni 2.8 sawa na 26.5%. Miradi 7 ya Sekta ya Maji inatarajiwa kutembelewa na Mwenge wa Uhuru Mkoani Kigoma
Kaulimbiu ya ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2019 ni " Maji ni Haki ya Kila mtu, tutunze vyanzo vyake na tukumbuke kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa