Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Albert Msovela amewataka wakuu wa Idara na Vitengo katika Halmashauri za Mkoa wa Kigoma kushrikiana na wafanayakazi walio chini ya idara zao kiutendaji ili kupata matokeo chanya katika kazi wanazozifanya za Utumishi wa Umma.
Msovela ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) uliofanyika Leo Desemba 15, 2022 katika Ukumbi wa NSSF, uliopo katika Halmashauri ya Manispaa Kigoma/Ujiji, ukiwa ni Mkutano wa pili wa Mwaka.
Amesema wakuu wa Idara na Vitengo wanapaswa kuwajengea uwezo watumishi walio chini yao ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa weledi, kasi na kiwango kinachotakiwa kuendana na mipango na malengo yaliyowekwa na Serikali yanayohitaji kuhitaji kufikiwa kiutendaji.
‘‘Kumekuwa na changamoto kubwa ya watumishi kukosa mahusiano mazuri na wakuu wao wa kazi huku wengine wakitekeleza majukumu bila kuwa na mipango kazi au kufanya kazi kwa kutumia uzoefu bila kuzingatia miongozo ya kazi hizo’’
Ameendelea kusisitiza kuwa, wakuu wa Idara na vitengo wanatakiwa kuendelea kuwa karibu na watumishi walio chini yao ili kuimarisha utendaji kazi na kuondoa migogoro ambayo inaweza kutatulika na kupafanya kazini kuwa sehemu yenye umoja na kusikilizana hali itakayoongeza ari ya utendaji kazi.
Aidha kupitia kikao hicho, wajumbe wamejadili utekelezaji wa Maazimio ya kikao kilichopita cha Tarehe 28 Januari 2022, kupokea na kujadili taarifa ya utoaji wa Huduma za Afya kimkoa, Shyghuli zilizotekelezwa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini, kazi zilizofanywa na Shirika la kidini la CARITAS-Kigoma, kwa Kipindi cha Julai hadi Oktoba 2022.
Kikao hicho kimehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa, baadhi ya Wah. Wabunge wa Mkoa wa Kigoma, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala, Wakurugenzi, Kamati ya Usalama Mkoa, Viongozi wa Dini na vyama vya Siasa, Wataalam kutoka Taasisi za Umma na Mashirika mbalimbali, Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa pamoja na wazee Maarufu.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa