Serikali, imeendelea kusisitoiza wakulima kuuza zao la pamaba kupitia vyama vya Ushirika vya Msingi ili kuondokana na wizi pamoja na usumbufu wanaopata kwa kuibiwa na
madalali wa zao hilo.Haya yamelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma wakati wa kuzindua Msimu wa ununuzi wa Pamba katika Kijiji cha Kanyonza Wilayani Kakonko.
Katika Msimu wa mwaka 2017/2018 takribani jumla ya ekari 2,932 zimelimwa kati ya hizo Wilaya ya Kakonko ekari 2,800 ,Kibondo ekari 12 na Kasulu ekari 251. Imeelezwa
kuwa Wilaya za Kibondo na Kasulu msimu huu ni wapili kulima zao la pamba, hivyo wananchi wa maeneo haya wamesisitizwa kuwa na mwamko wa kutumia fursa ya zao la pamba.
Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi na Maafisa Kilimo kuhakikisha wananchi wamahamasishwa kuongeza uzalishaji wa pamba kutoka wastani wa tani 2,932 kufikia lengo la tani
4,000 kwa mwaka hadi ifikapo mwaka 2020
Ni nia njema ya Serikali yetu ya awamu ya tano kuendeleza Sekta ya Kilimo cha pamba ili kiwe cha tija na kiweze kutoa mchango wake unaostahili katika kubadili hali ya
kiuchumi waliyonayo watanzania kwa ujumla ameongeza Maganga.
Mkoa wa Kihgoma una chama kimoja cha Msingi cha Ushirika wa Pamba ambacho ni Kanyonza. Kwa mujibu wa muongozo Na. 1 wa msimu 2018/2019 Pamba yote itakayovunwa
inatakiwa kuuzwa kwenye vyama vya ushirika vya msingi katika maeneo husika ili kumuepushia mkulima usumbufu na kumuhakikishia soko la uhakika.
Aidha ilikuwapunguzia wakulima usumbufu kunahaja ya kuanzisha vituo ambavyo vitahusika kununulia pamba za wakulima kwa kusimamiwa na chama cha ushirika cha msingi. Bei ya pamba kwa kilo moja itakuwa Tsh. 1,100.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa