Wananchi katika vijiji vya Kandaga na Mlela wilayani Uvinza mkoani Kigoma wameishukuru Serikali kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kwa kukamilisha Mradi wa Maji Mlela na kuwatoa kwenye adha ya kunywa Maji ya mito na visima hali iliyokuwa ikiwasababishia kuugua maradhi ya tumbo mara kwa mara.
Wakazi hao wamesema nyakati za kiangazi visima vilikuwa vikikauka na kulazimika kutumia maji ya mtoni ambayo hayakuwa salama kutokana na kuchafuliwa na mifugo pamoja na Shuguli nyine za kibinaadamu.
‘’Nyakati za mvua maji yalikuwa yakichafuka sana pia kiangazi visima vilikuwa vinakauka hali iliyokuwa ikitulazimu kutumia maji ya kwenye mito pamoja na mifugo na kusababisha kuugua maradhi ya tumbo mara kwa mara kutokana na jamii kutojenga mazoea ya kuchemsha maji ya kunywa’’ alisema Wiston Simon mkazi wa kijiji cha Mlela.
Upande wake Meneja wa RUWASA Wilaya ya Uvinza Mha. Bakari Kiwitu, amesema kukamilika kwa Mradi huo kumeondoa adha ya kutumia muda mrefu kwa ajili ya kufuata maji mitoni na badala yake wakazi hao watatumia muda huo kwa shughuli za Maendeleo.
Mha. Kiwitu amefafanua kuwa, Mradi wa Maji Kandaga unahudumia wananchi 11,978 wa vijiji hivyo kupitia vituo 37 vya kuchotea Maji pamoja na mabomba 27 yaliyovutwa na kutoa huduma hiyo kwenye makazi ya watu binafsi.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa