M
MKUU WA MKOA WA KIGOMA AKIFAFANUA JAMBO HUKU AKISILIZWA NA WADAU WA MAENDELEO KUTOKA TAASISI YA DANISH REFUGEE COUNCIL (DRC) WALIPOFIKA OFISINI KWAKE KWA AJILI YA KUSALIMIA KISHA KUTOA TAARIFA YA MPANGO WA UTEKELEZAJI MRADI WA HEWA YA UKAA MKOANI HAPA LEO SEPTEMBA 6, 2023.
Serikali mkoani Kigoma imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa Maendeleo ili kukabiliana uharibifu wa Mazingira na Athari zake.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye alipokutana na Ujumbe kutoka Shirika lisilo la kiserikali la Danish Refugee Council (DRC) kwa ajili ya kupokea Taarifa ya mpango wa jumla wa utekelezaji Mradi wa hewa Ukaa mkoani Kigoma.
Amesema katika maeneo wanayoishi wakimbizi, kumekuwa na Athari kubwa za kimazingira iliyosababishwa na ukataji holela wa miti kwa ajili ya kuni na Mkaa ili kupata nishati ya kupikia.
Amesisitiza kuwa, Mkoa upo tayari kuunga mkono utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimazingira ikiwemo upandaji wa miti, utoaji Elimu ya uhifadhi wa Mazingira pamoja na k uzalisha na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala.
Mkurugenzi mtedaji wa Taasisi ya DRC, Alfred Magehema amesema, Taasisi yake kwa kushirikiana na Kampuni ya Orsted ya nchini Denmark, wanatarajia kuanza kufanya utekelezaji wa Mradi wa Hewa Ukaa katika Wilaya za Kakonko, Kibondo na Kasulu ifikapo mwaka 2024.
Ameeleza kuwa, lengo la Taasisi yake ni kuhudumia wakimbizi pamoja na Jamii ya wakazi wenyeji inayoishi jirani na Kambi za wakimbizi kwa kutekeleza miradi ya kuboresha Maisha, Uhifadhi wa Mazingira pamoja na uzalishaji nishati mbadala ya kupikia.
Magehema amefafanua kuwa Taasisi ya DRC inaendelea kutekeleza kazi mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha shughuli za Kilimo, kutoa mafunzo ya ufundi Stadi na mikopo kwa wanawake na vijana, kutoa huduma za kisheria, ulinzi wa mtoto pamoja na uwezeshaji kiuchumi kwa watu wenye mahitaji maalum.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa