Na. Clinton Justin-KIGOMA
Mradi wa Afya Hatua unaotekelezwa na Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR), kupitia Kituo cha Kuthibiti na kuzuia Magonjwa Marekani (CDC), umetajwa kuwa ni miongoni mwa suluhisho muhimu katika kukabiliana na Virusi vya Ugonjwa wa UKIMWI Manispaa ya Kigoma Ujiji Mkoani hapa.
Mratibu wa Huduma za Afya ngazi ya Jamii kutoka Shirika lisilo la kiserikali Tanzania Health Protection Support (THPS) wilaya ya Kigoma mjini , Yethero Mgale amesema, mradi huo umekuwa chachu katika kuhamasisha ufuasi wa dawa za kufubaza maradhi ya UKIMWI huku akitoa wito kwa jamii kujitokeza kwa wingi kupata huduma za dawa kinga.
“Tunaomba jamii ijitokeze kwa wingi kupata huduma hizi, malengo yetu ni kuhakikisha kwamba ifikapo mwaka 2030 ,tunatokomeza kabisa maambukizi mapya ya VVU ” ,Amesema Yethero.
Mnufaika na mtumiaji wa dawa kinga aina ya Post Exposure Prophylaxis (PEP), Bi. Hadija Issa ambaye ni mkazi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji , amewashauri wanawake wanaoishi mazingira hatarishi ambayo ni vyepesi kupata maradhi hayo, kujenga tabia ya kutumia dawa kinga kwa ajili ya kujijengea usalama wao dhidi ya maambukizi wa virusi vya UKIMWI .
“Wanawake wenzangu muwe na ujasiri wakutumia dawa hizi kwa ajiri ya kujikinga na maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ’’.amesema Hadija
Kupitia mradi wa Afya Hatua chini ya Shirika la (THPS), Jamii katika halmashauri hiyo zinaendelea kuhamasishwa kuhusu umuhimu wa dawa kinga ,upimaji wa afya na matumizi ya huduma zinazosaidia kupunguza kasi ya maaambukizi , hatuaambayo ni muhimu kuelekea jamii yenye afya bora na isiyo na unyanyapaa.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa