Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameupongeza Uongozi wa Benki ya NMB Nchini kwa kuendelea kutoa Fedha kwa ajili ya Ufadhili wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo pamoja kuendesha Program ya uhifadhi wa Mazingira.
Makamu wa Rais ametoa pongezi hizo alipozungumzana Wananchi wa Wilaya hiyo baada ya kuzindua Tawi Jipya la Benki ya NMB katika Wilaya ya Buhigwe Mkoani hapa.
Amesema Benki hiyo imekuwa ikitoa Fedha nyingi kupitia gawio, ambazo kimsingi zimeendelea kutumika katika kutekeleza miradi mbalimbali nchini kwa lengo la kuwaletea Maendeleo wananchi.
Amesema serikali imekuwa ikitumia Fedha hizo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya Huduma za Jamii kama vile Maji, Umeme, Elimu, Barabara pamoja na Afya.
Dkt. Mpango ameendelea kufafanua kuwa, Benki ya NMB imeendelea kutumia fedha nyingi katika kufadhili mradi wa upandaji wa miti katika Maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kutunza Mazingira.
Kuhusu umuhimu wa kufunguliwa kwa Huduma hiyo ya kifedha wilayani Buhigwe, Dkt. Mpango amesema ‘’itawapunguzia kero ya kufuata huduma za kibenki mbali na maeneo yao ya makazi pamoja na kuwatoa wananchi kwenye mfumo usio rasmi wa kuhifadhi Fedha zao’’
‘’Baadhi ya wananchi walilazimika kufuata Huduma hii kwa umbali wa Km. 70, jambo ambalo lilisababisha baadhi ya wananchi kutunza Fedha kupitia mifugo, mashamba na hata kuzitunza ndani kwa kutumia utaratibu usio sahihi’’
‘’Niwasisitize viongozi wa NMB mhakikishe Benki hii inatoa fursa ya upatikanaji wa mikopo kwa wajasiriamali wadogo, vikundi vya wanawake pamoja na wakulima wadogo ili waweze kujiimarisha kiuchumi’’ ameendelea kusisitiza.
Aidha Dkt. Mpango amezielekeza Benki mbalimbali nchinikufanya utafiti ili kubainimaeneo yanayokidhi kuanzishwa huduma na kufungua matawi ya Benki hizo, mawakala na mifumo mingine itakayorahisisha utoaji na upatikanaji wa Huduma za kifedha.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amewaasa wakazi wa Wilaya ya Buhigwe kunza kutumia fursa zote za Huduma za kifedha zitakazotolewa na Benki hiyo kwa lengo la kujiletea Maendeleo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amewaasa wakazi wa Wilaya ya Buhigwe kunza kutumia fursa zote za Huduma za kifedha zitakazotolewa na Benki hiyo kwa lengo la kujiletea Maendeleo.
‘’Huduma za kibenki zitolewazo na Taasisi hii ya kifedha ni za uhakika na zimeendelea kugusa makundi yote yenye lengo la kupata huduma za mikopo midogo’’ amesema.
Philbert Mponzi ambaye ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Tanzania, amesema tawi la Benki hiyo lililozinduliwa Buhigwe ni la 229, huku Taasisi hiyo ikifanikiwa kuanzisha Mashine za ATM 780 pamoja na kuwezesha asilimia 95 ya miamala ya Fedha kufanyika nje ya Benki kwa lengo la kuongeza fursa za ajira kwa wananchi.
Mponzi amesema kuwa Taasisi yao itatoa Elimu ya masuala ya kifedha na kuibua ubunifu kwa lengo la kuwajengea uwezo wananchi katika kujiongezea kipato na kuimarisha uchumi wao binafsi na mkoa kwa ujumla.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa