MKUU WA MKOA WA KIGOMA CGF(Rtd) THOBIAS ANDENGENYE AKIWASALIMIA WANAKIGOMA WALIOJITOKEZA KATIKA UWANJA WA UMOJA KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA KASULU KABLA YA KUWAHUTUBIA IKIWA NI KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR KIMKOA.KATIBU TAWALA MKOA WA KIGOMA HASSAN RUGWA AKIZUNGUMZA NA WANAKIGOMA WALIOJITOKEZA KUSHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO KATIKA UWANJA WA UMOJA MJINI KASULU.BAADHI YA WATENDAJI WA SERIKALI WALIOJITOKEZA NA KUSHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO HAYO MJINI KASULU LEO TAREHE 26, APRILI 2026.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kamishna Jenerali Mstaafu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye amesema Maendeleo yaliyofikiwa na Taifa la Tanzania yametokana na msingi wa Umoja, Amani na Mshikamano uliojengwa na waasisi wa Taifa.
Amesema kuimarika kwa Uchumi wa nchi kunatokana na Mazingira bora pamoja na mahusiano mazuri yaliyowekwa na viongozi hao kunasababisha kuendelea kushuhudiwa kwa uboreshwaji mkubwa wa miundombinu ya kutolea huduma za Jamii ikiwemo Afya, Maji, Umeme, Nishati ya Umeme, uwezeshaji kiuchumi pamoja na kuimarisha Mazingira wezeshi ya uwekezaji ndani nan je ya nchi.
‘’Wanakigoma leo wanashuhudia upatikanaji wa uhakika wa huduma za maji, umeme, uwepo miundombinu ya kitaaluma, kuboreshwa kwa miundombinu ya usafiri na usafirishaji, yote haya yakiwa ni matunda ya mshikamano unaotokana na Muungano wetu’’ amesema.
Ameendelea kusisitiza kuwa, kila mwananchi anapaswa kuulinda muungano na kuudumisha ili kuliweka Taifa katika hali ya Amani na utulivu jambo litakalotoa fursa kwa wananchi kujikita katika utendaji kazi na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Tumeshuhudia Amani, utulivu pamoja na usalama ndani ya nchi yetu huku serikali zote mbili zikiendelea kujiendesha kwa uwazi chini ya misingi ya kisheria, demokrasia, utawala bora kutokana na wananchi kuwa na uelewa mzuri kuhusu dhana ya uwajibikaji na kujengeana heshima kwa ngazi na rika zote.
Upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Hassan Rugwa amesema mkoa umeendelea kushuhudia matunda ya Muungano ikiiwa ni pamoja na maendeleo makubwa katika Sekta mbalimbali ikiwemo maboresho katika sekta za utoaji wa Huduma za Jamii.
Aidha amewashukuru wakazi wa mkoa wa Kigoma jitihada mbalimbali wanazozifanya kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi na kujiletea maendeleo.
Naye Mkazi wa Mji wa Kasulu Ambaye pia ni Chifu wa Kimila Alfredy Kimenyi amesema ni jukumu la Wazazi kuwaelimisha na kuwarithisha watoto wao misingi ya Muungano ili kulifanya Taifa lizidi kuwa Imara na lenye maendeleo makubwa katika miaka ijayo huku likiendelea kuwa lenye Amani na utulivu.
Maadhimisho ya Miaka sitini ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kimkoa yamefanyika katika Uwanja wa Umoja uliopo katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu na kuhudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma Mhe. Hassan Rugwa, Wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa, wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa wilaya, wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, wakuu wa Taasisi za Umma, Viongozi wa Vyama vya Siasa pamoja na viongozi wa Dini.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa