Mkuu wa Mkoa awataka wakandarasi kukamilisha Miradi ya Maji haraka
Posted on: April 19th, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Brigedia Jenerali Emanuel Maganga (mstaafu) amewataka wakandarasi wanaojega miradi ya Maji Mkoani Kigoma Kukamilisa miradi hiyo hara ili wananchi waanze kupata Huduma ya maji.
Amesema haya katika nyakati tofauti wakati wa ziara yake ya kikazi katika Wilaya za Kibondo, Kigoma na Uvinza yenye lengo la kukagua miradi na kuamasisha maendeleo kwa Wananchi Mkoani Kigoma.
“Hakuna sababu ya kuchelewesha miradi ya maji kwa sasa kwani Serikali imesatoa fedha nyingi kukamilisha miradi hii, malizeni kazi haraka ili maji yapatikane kwa wananchi” alisema Maganga.
Katika hatua nyingine Mhe. Maganga amewataka wanchi kuitunza na kuithamini miradi ya maji pindi inapokabidhiwa kwa matumizi yao kwani Serikali inatumia fedha nyingi kuhakikisha wananchi wanapata maji maji safi na salama kwa umbali mdogo kama ilivyoainishwa katika Malengo endelevu ya Milenia.