Mkuu wa Mkoa awataka Viongozi wa Dini kuilinda Amani Mkoani Kigoma
Posted on: June 20th, 2017
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amewaomba viongozi wa dini nawananchi wa Mkoa wa Kigoma kuendelea kuiaminini na kuziunga mkono juhudu za Serikali ya awamu ya tano chini ya Uongozi wa Rais John Pombe Magufulina katika kuleta maendelo.
Maganga aliyasema hayo wakati wa kula futari aliyoiandaa mahsusi nyumbani kwake Ikulu ndogo Mkoani Kigoma kwa ajili ya kukutana na waislamu pamoja na viongozi mbalimba wa Serikali ya Mkoa.
Pamoja na mambo mengine Manganga alisisitiza suala la ulinzi na usalama, na Amani kuwa ni vitu vya Msingi kwa raia wa kitanzania kuvisimamia. Alieleza kuwa kumekuwepo na watu kulalamika kuwa kila mara wanahojiwa na vyombo vya dola juu ya urai, alisema hilo ni jukumu la vyombo hivyo kuhakikisha ukweli wa raia pale vinapoona inafaa hivyo wananchi wasisite kutoa ushirikiano
Amewaomba waumini wa dini ya kiislamu kupitia mfungo mtukufu wa Ramadhani wadumu katika sala na kuliombea taifa Amani na Mshikamano.