Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. Mst. Emanuel Maganga amewaagiza Wakuu wa Wilaya kutomuonea aibu mtu yoyote atakayekwamisha zoezi la ukusanyaji wa Mapato katika Halmashauri kwa kwaslahi yake ama ya kisiasa au ya kibiashara,
Mkuu wa Mkoa Maganga amesema hayao mara baada ya Kuwaaapisha Wakuu wa wilaya za Buhigwe na Kasulu, amesema kazi kubwa ya kwanza kama wakuu wa Wilaya wanakazai ya kusimamia ukusanyaji wa mapato katika Halmasauri ili Serikali ipate kodi. " kumekuwa na watu wanaingiza ziasa katika suala la ukusanyaji mapato na hivyo kuathiri mapato ya ndani ya Halmashauri ninasema mtu yeyote asilete siasa au maslahi yake binafsi wakuu wa Wilaya mkimgundua mtu wa aina hiyo awekwe ndani na kupelekwa Mahakamani maramoja kwa kuhujumu uchumi wa nchi" alisisitiza Maganga.
Kwa mara nyingin Mhe. Maganga amekazia suala la Madiwani wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kujirekebisha kabla Serikali ya Serikali kuvunja Manispaa hiyo ambapo Baraza la Madiwani limekuwa na mvutano mkubwa kati ya Watendajikatika suala zima la ukusanyaji mapato na kuifanya manispaa kuwa tegemezi kwa Serikali kuu kwa asilimia 96 licha ya kuwa na vyanzo vingi vya mapato kuliko Halmashauri nyingine Mkoani Kigoma.
Kwa upande wao Wakuu wa Wilaya Lt. Kanali Michael Masala Ngayalina wa Wilaya ya Buhigwe na Kanali Simon Mahenge Anange Mkuu wa Wilaya ya Kasulu wameahidi kuchapa kazi, na kutoa ushirikiano wa dhati katika kusukuma maendeleo ya Wananchi wa Wilaya wanazoziongoza.
Adish, Mhe. Mkuu wa Mkoa amewapa kazi wakuu wa Wikaya wote Mkoan humo kuanzia utaratibu wa mfumo wa ulinzi wa Nyumba kumi kumi ili kuimarisha suala la Ulinzi katika ngazi ya Mtaa hadi Wilaya.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa