Wananchi wamehimizwa kuunga mkono juhudi za serikali za kufufua zao la Pamb ili kuwainua kiuchumi na kuondokana na hali ya Umaskini. Haya nyamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig.Jen. (mst.) Emannuel Maganga wakati akihudumia shamba lake mfan la zao la Pamba Wilayani Kakonko katika Kijiji cha Kanyonza.
Mkuu wa Mkoa amesema ameona ni vyema kuunga mkoni agizo la Mhe. Waziri Mkuu wa Tanzania kwa kutoa mfano ili kwa mikoabyote kufufua mazao matano ya Kimkakati ambayo ni Pamba, mbali na kuinua hali za wananchi kiuchumi zao la pamba ni mali ghafi ambayo itachochea viwanda vyetu hapa nchini hivyo kuzalisha ajira kwa wananchi wetu.
Zao la Pamba katika Mkoa wa Kgoma hustawi sana katika Wilaya ya Kakoko na Kibondo. Naye Mkuu w Wilaya ya Kakonko Kanali. Hosea Ndagala amesema Kakonko imejiapanga kuweka mikakati ya kuhakikisha unakuwa miongoni mwa Wilayakinara katika kikimo cha zao la pamba.
Wananchi Mkoani Kigoma wamehimizwa kufufua zao la Pamba ambalo litawaongezea kipata na upunguza kasi ya kuuza vykula kwa mahitaji yao.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa