Taasisi ya kupambana na Rushwa TAKUKURU Mkoani Kigoma imeagizwa kuwachunguza kuchunguza na kutoa taarifa ndani ya Wiki tatu atumishi 10 wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko kutokana na sintofahamu ya kutokikamilika kwa wakati Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Gwanumpu Wilayani Kakonko.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig.Gen.(Mst.) Emmanuel Maganga alipokutana na Viongozi pamoja na watendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Kakonko kwa lengo la kutaka kujua kwa nini Kituo hicho hakijakamilika licha ya Serikali kutoa fedha na kwamba Ujenzi wa Kituo hicho ulipaswa kukamilika mwezi Desemba 2018.
Takribani watumishi 10 kutoka katika idara mbalimbali za Halmashuri ya Wilaya ya Kakonko wanahusishwa na ucheleweshwaji wa kumalizika kwa Kituo hicho ikiwemo kukiuka sheria, kanuni na taratibu za Manunuzi, pamoja na baadhi yao kujiingiza kwenye kwenye Kamati ya Ujenzi na hivyo na kusababisha ubadhirifu.
Siku moja kabla ya kikao na Watendaji Mkuu wa Mkoa alifanya Ziara ikiwa pamoja na kukagua miradi itakayopitiwa na Mwenge wa Uhuru ndipo akakutana na madudu ambayo yalimfanya aitishe kikao cha dharuala na kutoa maelekezo makali kwa wanaokamisha kukamilika kwa Kituo hicho.
" Leo ni Mara ya tatu natembelea Kituo hiki halafu kila nikija nakuta bado hakijakamilika nataka nijue nani na nini kimekwamisha, haiwezekani Serikali itoe fedha halafu watu wachache tu mtukwamishe" alisema Maganga.
Aidha pamoja na TAKUKURU kupewa jukumu la kubaini waliohusika katika viashiria vya ubadhirifu Mkuu wa Mkoa amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri kuangalia namba ya kuwaondoa watumishi waliotajwa katika mlolongo mzima wa ukwamishaji katika kukamilisha Ujenzi huo, na kwamba ndani ya wiki moja Kituo hicho kiwe kimekamilika na kuanza kuwahudumia wananchi wa Gwanumpu.
Serikali imekwishatoa Shilingi milioni 500 kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Gwanumpu, hadi sasa ukamilishwaji umeelezwa kufikia asilimia 90 huku fedha iliyobaki hadi sasa ni Milioni 30.
==≠==≠====≠======≠==========≠
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa