Mkuu wa Mkoa amemwelezea Bw. Grandi kuwa Mkoa wa Kigoma ambao unahifadhi idadi kubwa ya wakimbizi bado unapata changamoto nyingi za masuala ya wakimbizi, hususani katika masuala ya Urejeaji wa hiari wa wakimbizi katika nchi yao Burundi umekuwa ni wa kususasua licha ya makubaliano ya Pande tatu yaliyofanyika Nchini Burundi Machi 2018.
Hali ya mazingira pia ilielezwa kuendelea kuwa mbaya kutokana na wakimbizi Mkoani Kigoma kuendelea kutmia kuni kama nishati kuu ya kupikia kitu ammbacho kinasababisha uharibifu wa misitu na mazingira.
Aidha amesema Mkoa wa Kigoma unaendele kushirikiana na Shirika la kuhudumia wakimbizi Dunia kuhakikiasha wakimbizi wanarejea nchini kwao kwa kuzingatia utu na heshma. Maganga amesisitiza kuwa bado kunahaja ya shirika la Wakimbizi duniani kuharakisha kuwarejesha kwao wakimbizi waliakwisha jiandikisha kwa hiari kurejea kwa hiari nchin mwao.
Kwaupande wake Bw. Grand amesema amfika Mkoani Kigoma kujionea shughuli mbalimbali ikiwemo utekelezwaji wa makubalinao yaliyofikiwa kati ya Serikali ya Tanzania na UHNCR juu ya wakimvizi waliopo Mkoani Kigoma hususani urejeaji wao katika nchi yao asili.
Grandi amesema kuwa bado Shirika la UNHCR litaendelea kuwerejesha wakimbizi nchi kwao, japo kwa muda Zoezi lilisuasua kutokana na kukosekana kwa fedha na sasa tayari fedha zimekwishapatoikana kundi la kwanza la wakimbizi litaanza kuondoka hivi karibuni.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa