Mkutano wa sita (6) wa tume ya kudumu ya kati ya Tanzania na Burundi unafanyika kwa siku tatu Mkoani Kigoma, mkutano huo wenye lengo la kuboresha ushirikiano wa Tanzania na Burundi katika maeneo ya Siasa na Diplomaia, Ulinzi na Usalama, Maendeleo ya Miundombinu, Ushirikiano wa kiuchumi na ushirikiano katika sekta za kijamii.
Mkutano huu ni utekelezaji wa maelekezo ya Mh Rais DKt John Pombe Joseph Pombe Magufuli wakati wa ziara yake Mkoani Kigoma ambapo tarehe 19 September 2020 alikutana na kufanya mazungumzo na Mhe. Evariste Ndayishimile, Rais wa Burundi na kukubaliana Tanzania na Burundi kufanya mkutano wa tume ya pamoja ya kudumu (Joint permanent Commission).
Kufuatia maelekezo hayo tume ya Pamoja ya kudumu kati ya Tanzania na Burundi zimeanza mkutano wa sita (6) leo 3 Machi 2021 Mkoani Kigoma. Mkutano huo utafanyika chini ya Mhe. Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi (Mb) Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mh Balozi Albert Shingiro, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi.
Akizungumza leo Machi 2, 2021 wakati wa kuanza kwa vikao vya Wataalamu na Makatibu Wakuu mkoani Kigoma Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Balozi Brig. Gen. Wilbert Ibuge amesema mkutano huo utawakutanisha makatibu wakuu wa sekta tofauti na baadaye mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Tanzania na Burundi.
Balozi Kanali Ibuge ameeleza kuwa Tanzania imekuwa mwenyeji wa Mkutano huu kwa miaka 15 ambapo mkutano wa tano ulifanyika jijini Dar es Salaam mwaka 2006.
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa