Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Misaada ya Kimataifa la Marekania USAID Bw. Andy Karas amesema amefurahishwa na utekelezaji wa miradi mbalimbali inayo fadhiliwa na Shirika hilo.
Karas Amesema hayo alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emmanuel Maganga ofisini kwake.
Tunafurahi kuona miradi mbalimbali tunayoifadhili inatekelezwa Mkoani Kigoma kwa manufaa ya wanachi kama inavyokusudiwa.
Ameongeza kuwa USAID itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuzingatia vipaumbele na Mipango ya Serikali ya Tanzania.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brig. Jen. Maganga ametoa shukrani kwa USAID kwa juhudi wanazozifanya katika kuendeleza Mkoa wa Kigoma hususan katika masuala ya Afya, Elimu na Mazingira
MKOA WA KIGOMA
Anuani: S.L.P 125
Simu: 0282802330
Simu ya kiganjani: +255766853404
Barua Pepe: ras@kigoma.go.tz / ras.kigoma@tamisemi.go.tz / info@kigoma.go.tz
Hakimiliki©2018. Mkoa wa Kigoma. Haki zote zimehifadhiwa