MKURUGENZI EPZA ASISITIZIA SUALA LA UWEKEZAJI KATIKA VIWADA MKOANI KIGOMA
Posted on: October 25th, 2017
Suala la viwanda kuelekea uchumi wa kati sio jambo la kisiasa, viongozi na watendaji hawapaswi kuteteleka katika kulizungumzia na kulisimamia kwa nguvu zote.
Amesema Mkurugenzi Mkuu wa Malmaka ya Mauzo ya nje ‘Expot Processing Zone Authority’ (EPZA) Kanali (Mst) Joseh Leon Simbakali wakati akizungumza na Viogozi na watendaji katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, wakati wa kukagua maendelo ya eneo maalum la uwekezaji Mkoa wa Kigoma KiSEZ.
Serikali ya awamu ya tano imedhamiria kuleta mabadiliko katika sekta ya viwanda ambayo ndiyo njia kuu ya kuifanya nchi kuwa na uchumi wa kati.
Makosa ya zamani yaliyojitokeza hadi kupelekea viwanda vilivyokuwepo nchini kufa, kuuzwa na kubinafsisha Serikali inayafahama na kwamba hakuna hali kama hiyo inaweza kujitokeaza wala kujirudia.
Mhe. Simbakalia amesema Mkoa wa Kigoma unafursa nyingi kutokana na kuwa lango kuu la Nchi za Burundi, Congo, zaire kwa bashara. Hivyo serikali inafanya jitihada kubwa kuhakikisa miundombinu ya kuvutia uwekezaji Mkoani Kigoma inaimarika ili Kigoma iwe kitovu cha kibiashara eneo la maziwa makuu.